Friday, December 2, 2011

R.I.P Mr Ebbo



Msanii Maarufu aliyepata kutamba sana na nyimbo zake za KAMONGO na MIMI MMASAI BWANA, Abel Loshilaa Motika na kujilikana sana kwa jila la Mr Ebbo amefariuki dunia.

Ebbo msanii aliyejizolea mashabiki wengi hapa nchini kwa staili ya muziki wake aliokuwa akifanya wenye lafudhi ya kimasai , Mr Ebbo ameaga dunia usiku wa kuamkia leo. Mr Ebbo alikuwa anasumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na amefariki akiwa nyumbani jijini Arusha katika eneo la masai camp familia yake ianapoishi hata hivyo inasemekana aliwahi kulazwa katika hospitali moja huko Usa River.
Mr Ebbo wakjati wa uhai wake alikuwa akiishi jijini Tanga na kufanya shughuli zake za Muziki huko ikiwa ni pamoja na kufungua Studio ya Muziki ya motika record .

mungu ailaze pema roho ya marehemu

No comments:

Post a Comment