Thursday, March 29, 2012

Rais Amadou Toumani Toure Mali asema yuko salama


Kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea wiki moja sasa  nchini Mali ,Rais aliyepinduliwa nchini Mali  Amadou Toumani Toure, amesema yuko salama katika mji mkuu Bamako, na hashikiliwi na wanajeshi waliompindua wiki iliyopita.
Akizungumza na shirika la habari la Ufaransa, AFP, alisema yeye na familia yake wako katika hali nzuri, na anafuatilia hali ya mambo inavyoendelea nchini mwake. Rais Toure amesema anaiombea Mali iendelea kuwa na amani na demokrasia.
Tangu alipopinduliwa tarehe 22 machi, Amadou Toumani Toure amekuwa hajulikani aliko, na wasi wasi juu ya hatima yake umekuwa ukiongezeka. Wakati huo huo, shinikizo dhidi ya wanajeshi waliofanya mapinduzi hayo linazidi.
 Jumuiya ya uchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS, jana ilituma ujumbe wa kijeshi nchini Mali, kutayarisha ziara ya ujumbe mwingine wa Kisiasa utakaoongozwa na Rais wa Burkina Faso, Blaise Compaore. ECOWAS inataka kuundwa kwa serikali ya mpito nchini Mali itakayoongozwa na spika wa Bunge Dioncounda Traore.  

No comments:

Post a Comment