Thursday, March 29, 2012

Waethiopia waachiwa huru nchini Yemen



Polisi nchini Yemen wamewakomboa wahamiaji haramu 21 wakiethiopia ambao waliteswa na  watu waliokuwa na silaha, ili kuwalazimisha jamaa zao walioko Saudi Arabia kutuma fedha kama malipo ya fidia.

 Taarifa ya Wizara ya ndani ya Yemen imesema wahamiaji hao ni pamoja na wanawake 14 , walikuwa wakizuiliwa ndani ya nyumba moja katika mji wa Hajja, karibu na mpaka  na Saudi Arabia. 

 Polisi wa Yemen walilivamia jengo hilo na kuwakamata wateka nyara watatu wakiwemo wawili waliokuwa wakiwatesa Waethiopia hao kwa kutumia waya wa umeme na  minyororo. 

Raia hao wa Ethiopia sasa wamekabidhiwa kituo cha  wakimbizi cha Umoja wa mataifa ili warudishwe nyumbani.

No comments:

Post a Comment