WAZIRI sita kati ya wanane waliokuwa wakilalamikiwa na kutakiwa waondolewe katika Baraza, wameachwa katika Baraza jipya.
Akitangaza mabadiliko katika Baraza lake jana Ikulu, Dar es Salaam, Rais Jakaya Kikwete aliwaondoa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami.
Wengine ‘waliotoswa’ ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda na wa Uchukuzi, Omar Nundu.
Sura mpya katika Baraza hilo ni Dk Abdallah Kigoda anayekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara; Dk William Mgimwa anayekuwa Waziri wa Fedha na Profesa Sospeter Muhongo anayekuwa Waziri wa Nishati na Madini.
Waliopandishwa hadhi kuwa mawaziri kamili ni Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye amehamishwa kutoka Ujenzi na sasa anakuwa Waziri wa Uchukuzi; Dk Fenella Mukangara ambaye sasa anakuwa waziri kamili wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kwa upande wa mawaziri waliorejea katika nafasi zao, Rais aliwataja Stephen Wasira anayeendelea na nafasi yake ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu.
Wengine ni katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi ni Samia Suluhu (Muungano), na Terezya Huvisa anaendelea na Mazingira na katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mary Nagu anaendelea na Uwekezaji na Uwezeshaji, huku William Lukuvi akiendelea na Sera na Hawa Ghasia anashughulikia Tamisemi.
Samuel Sitta anaendelea na Ushirikiano wa Afrika Mashariki huku Bernard Membe akiendelea na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa; John Magufuli anaendelea na Ujenzi wakati Dk. Shukuru Kawambwa akiendelea na Elimu. Kwa upande wa Maendeleo ya Jinsia na Watoto, Sophia Simba anaendelea;
Dk Mathayo David Mathayo anaendelea na Mifugo na Uvuvi, Gaudentia Kabaka amebaki Wizara ya Kazi na Ajira, Makame Mnyaa Mbarawa anabaki na Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Profesa Anna Tibaijuka anaendelea na Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waliobadilishwa ni Celina Kombani ambaye anakwenda Ofisi ya Rais kushughulikia Utumishi na George Mkuchika ambaye naye anakwenda huko kushughulikia Utawala Bora.
Hawa Ghasia amepelekwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako anachukua nafasi ya zamani ya Mkuchika ya Tamisemi; Shamsi Vuai Nahodha amehamia Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa huku Hussein Ali Mwinyi akihamishiwa Afya na Ustawi wa Jamii. Katika Wizara ya Katiba na Sheria, Mathias Chikawe amepelekwa huko, huku Dk Emmanuel Nchimbi akihamishiwa Mambo ya Ndani ya Nchi na Profesa Jumanne Maghembe akipelekwa Maji.
Kwa upande wa Utalii, Hamis Kagasheki amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii na Profesa Mark Mwandosya ambaye anakuwa Waziri asiye na Wizara Maalumu. Mawaziri waliopandishwa kutoka unaibu ni Dk. Harrison Mwakyembe kutoka Ujenzi kwenda Uchukuzi, Dk. Fenella Mukangara amepanda katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo alimokuwa na huku Christopher Chiza naye akipanda katika Wizara ya Kilimo, Ushirika na Chakula. Kwa upande wa manaibu, Athuman Mfutakamba ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi amefuata nyayo za Waziri wake Nundu kung’oka.
Sura mpya kwa upande huo ni George Simbachawene ambaye anakuwa Naibu Wizara ya Nishati na Madini, Saada Mkuya Salum anakuwa Naibu Wizara ya Fedha; Januari Makamba, Naibu Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia na Dk. Charles Tizeba anayekuwa Naibu Uchukuzi.
Wengine ni Charles Kitwanga anayekwenda kuwa Naibu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk Binilith Mahenge anakwenda Wizara ya Maji na Stephen Masele anayekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Amos Makalla anayekuwa Naibu Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Manaibu wengine wapya ni Angela Kairuki anayekwenda Katiba na Sheria na Janet Mbene anayekwenda Wizara ya Fedha na Dk Seif Suleiman Rashid Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Waliobadilishwa ni Adam Malima anayekwenda Kilimo, Pereira Silima anayekwenda Mambo ya Ndani; Gregory Teu, Biashara na Viwanda; Lazaro Nyalandu, Maliasili na Utalii na Gerson Lwenge, Wizara ya Ujenzi.
Waliosalia katika nafasi zao ni Dk Makongoro Mahanga (Kazi na Ajira); Mahadhi Maalim (Mambo ya Nje); Goodluck ole Medeye (Ardhi); Ummi Mwalimu (Watoto); Philipo Mulugo (Elimu) na Dk Juma Abdulla Juma (Afrika Mashariki).
Wengine ni Majaliwa Majaliwa na Aggrey Mwanri ambao wanaendelea na majukumu yao katika Ofisi ya Waziri Mkuu -Tamisemi na Benedict ole Nangoro (Mifugo na Uvuvi). Mawaziri hao wataapishwa keshokutwa Ikulu, Dar es Salaam.

Source: Habarileo.
No comments:
Post a Comment