Mladic
anashitakiwa kwa kuongoza mauaji ya kikatili ya Waislamu 8,000 wengi wao vijana
na watu wazima huko Srebrenica mnamo mwaka wa 1995. Hayo ndiyo mauaji ya
kikatili zaidi tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia.
Ratco
Mladic ambaye sasa ana umri wa miaka 70, ndiye mhusika wa mwisho katika vita
vya eneo la Balkan katika miaka ya tisini kufunguliwa mashitaka katika mahakama
ya Kimataifa ya Uhalifu kwa iliyokuwa Yugoslavia mjini The Hague.
Anatuhumiwa
kwa kuchochea siyo tu wiki nzima ya mauaji ya kikatili mjini Srebrenica, bali
pia kuzingirwa Sarajevo kwa miezi 43 ambapo zaidi ya watu 10,000 waliuwawa na
walenga shabaha, na makombora.
No comments:
Post a Comment