TAMASHA
la saba la vyombo vya babari Kanda ya Kaskazini, linatarajiwa kufanyika
Julai mosi, mwaka huu katika viwanja vya General Tyre mjini Arusha.
Katibu wa chama cha Waandishi wa habari za michezo na Burudani mkoani Arusha(TASWA Arusha) Mussa Juma amesema Tamasha hilo mwaka huu, linatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa.
Amesema katika tamasha hilo, ambalo uratibiwa na kampuni ya Ms Unique Promotion , litashirikisha wanahabari wa Arusha na Kanda ya Kaskazini, pamoja na Dar es Salaam.
Amesema timu nyingine ambazo zinatarajiwa kushiriki ni TBL Arusha, PEPSI,CRDB, NMB,Wazee Klabu, Kitambi Noma,Vodacom, Exim Bank,NSSF Arusha na nyingine kadhaa.
"mwaka huu tunatarajia mchuano utakuwa ni mkali hasa katika soka ambapo bingwa mtetezi ni Radio 5"amesema Juma.
Amesema kabla ya tamasha kutakuwa na semina ya wanahabari wa michezo kanda ya kaskazini.
Hata hivyo, amesema bado chama hicho, kinafanya mazungumzo na wadhamini mbali mbali ni kufanikisha tamasha hilo la kila mwaka.Wakati huo huo,Chama cha waandishi wa habari na michezo mkoa wa Arusha(TASWA- ARUSHA), kimetoa salamu za pole kwa familia ya aliyekuwa, Mhariri wa habari za michezo wa gazeti la Mtanzaia Rachel Mwiligwa ambayealifariki mwishoni mwa wiki na kuzikwa.
Katika
taarifa ya TASWA Arusha kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Katibu
wake, Mussa Juma, juziilisema kifo cha Rachel ni pigo kwa familia
yake, wanahabari na gazeti la Mtanzania.
"sisi kama TASWA Arusha tumepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwanahabari mwenzetu Rachael ambaye alikuwa nguli katika masuala ya michezo"alisema Juma
Rachael alikumbwa na umauti usiku wa kuamkia ijumaa kwenye hospitali ya Mwananyara Jijini Dar na amezikwa juzi.
Katibu wa chama cha Waandishi wa habari za michezo na Burudani mkoani Arusha(TASWA Arusha) Mussa Juma amesema Tamasha hilo mwaka huu, linatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa.
Amesema katika tamasha hilo, ambalo uratibiwa na kampuni ya Ms Unique Promotion , litashirikisha wanahabari wa Arusha na Kanda ya Kaskazini, pamoja na Dar es Salaam.
Amesema timu nyingine ambazo zinatarajiwa kushiriki ni TBL Arusha, PEPSI,CRDB, NMB,Wazee Klabu, Kitambi Noma,Vodacom, Exim Bank,NSSF Arusha na nyingine kadhaa.
"mwaka huu tunatarajia mchuano utakuwa ni mkali hasa katika soka ambapo bingwa mtetezi ni Radio 5"amesema Juma.
Amesema kabla ya tamasha kutakuwa na semina ya wanahabari wa michezo kanda ya kaskazini.
Hata hivyo, amesema bado chama hicho, kinafanya mazungumzo na wadhamini mbali mbali ni kufanikisha tamasha hilo la kila mwaka.Wakati huo huo,Chama cha waandishi wa habari na michezo mkoa wa Arusha(TASWA- ARUSHA), kimetoa salamu za pole kwa familia ya aliyekuwa, Mhariri wa habari za michezo wa gazeti la Mtanzaia Rachel Mwiligwa ambayealifariki mwishoni mwa wiki na kuzikwa.
"sisi kama TASWA Arusha tumepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwanahabari mwenzetu Rachael ambaye alikuwa nguli katika masuala ya michezo"alisema Juma
Rachael alikumbwa na umauti usiku wa kuamkia ijumaa kwenye hospitali ya Mwananyara Jijini Dar na amezikwa juzi.
No comments:
Post a Comment