Mbunge
wa Ubungo (Chadema), John Mnyika akiingizwa na askari wa bunge kwenye
gari baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru atolewe nje ya viwanja vya
bunge baada yambunge huyo kugoma kufuta kauli yake kuwa Rais Jakaya
Kikwete ni dhaifu, wakati akichangia hotuba ya bajeti ya serikali kwa
mwaka wa fedha 2012/13, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
Mussa Juma, Dodoma na Fedelis Butahe, Dar BUNGE
jana lilichafuka tena baada ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kusema
kuwa Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu, kauli ambayo ilisababisha Naibu
Spika, Job Ndugai kuamuru atolewe bungeni.
Mnyika alitoa kauli
hiyo wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13,
ambapo alieleza kuwa analazimika kusema Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu,
wabunge ni wazembe na nchi imefika hapa ilipo kutokana na upuuzi wa
Chama cha Mapinduzi (CCM).
"Mimi nasikitishwa na jambo moja,
tumefika hapa kutokana udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa bunge na
wabunge na tumefika hapa kutokana na upuuzi wa CCM, nasema hivi nina
ushahidi.” Lukuvi/ Ndugai Kauli hiyo ya Mnyika ndio ilichafua
hali ya hewa bungeni, ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Bunge na Uratibu, William Lukuvi ndipo alisimama na kuomba mwongozo wa
Spika. “Nataka kumbukusha Mnyika, kutokana na kauli zake, kwa kutumia
kanuni ya 64 (d) ambayo inaeleza mbunge yeyote hatatumia jina la Rais
kwa dhihaka katika mjadala au kulishawishi bunge kwa jambo lolote,”
alisema Lukivi.
Aliendelea kufafanua kuwa, “Lugha kwamba Rais
Kikwete ni dhaifu, CCM ni wapuuzi nilikuwa naomba, Mheshimiwa Mnyika,
miongoni mwa watu ninaowaheshimu sana, nadhani katika hili, amepotoka
naomba afute kauli yake.” Baada ya kauli hiyo ya Lukuvi, Ndugai
alifafanua zaidi kuhusu jambo hilo akisema ni kweli kanuni inajieleza
vizuri sio tu katika maneno yake pia amelisema vibaya Bunge hilo na
kumtaka afute kauli hiyo.
Mnyika alisimama na kuomba apewe nafasi
ya kufafanua kauli yake ya kwanini Kikwete ni Rais dhaifu, lakini Naibu
Spika, alimuomba afute kauli yake, kitu ambacho mbunge huyo aligoma
kufanya, badala yake akasisitiza bunge limpe nafasi ya kufafanua. Kutokana na uamuzi wa kumtimua Mnyika bungeni.
Ndugai
alisema mbunge anapotoa lugha ya matusi au maudhi na akatakiwa na kiti
cha Spika afute kauli yake na bado akagoma, ni mamlaka kwa kiti hicho
kumtoa nje ya bunge katika muda uliosalia au hata kumsimamisha
asihudhurie vikao vitano vya bunge. Ndugai aliamuru walinzi wamtoe Mnyika nje mara moja na kumzuia asishiriki shughuli yoyote ya bunge hadi kesho saa 3:00 asubuhi.
“Ndugu
wabunge tunaongozwa kwa utaratibu, nikitoa uamuzi wangu kwa Kanuni ya
73 (2), ambayo inaeleza kuwa, mbunge au waziri atakayetoa lugha ya
maudhi atatatakiwa na Spika ajirekebishe na akikataa atakaa nje kwa muda
wote ulisalia katika kikao cha siku hiyo. Nikiwa Naibu Spika
ninayejiamini, uamuzi ambao nauchukua sasa, Askari mliopo hapa naagiza
mumtoe nje mheshemiwa Mnyika mara moja,” aliagiza Ndugai.
Kabda
ya tukio hilo, Mnyika alichangia bajeti hiyo kwa maneno makali dhidi ya
wabunge wa CCM wanavyopigania bajeti ya Serikali isiyotekelezeka, huku
akiwafananisha na mtu asiye na akili timamu (chizi), kwamba yeye
akiendelea kupambana nao ndio ataonekana chizi zaidi. “Mtu ukiwa
unamkimbiza chizi wewe ndio utaonekana chizi zaidi, hivyo siungi mkono
na waache machizi waendelee na uchizi wao,” alisema.
Kauli hiyo
ya Mnyika inaonekana kutaka kujibu mapigo ya kikao cha juzi ambapo
mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba wakati akichangia
bajeti, alisema kuwa wapinzani ni wanafiki, waongo, wana mapepo na
wanapaswa kuombewa na kupimwa akili.
Alisema bajeti hiyo
haiendani na Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano, ambao ulisainiwa na Rais
Kikwete na pia haiendani na Ilani ya Uchaguzi ya CCM, hivyo akashangaa
kauli za wabunge wa chama tawala kuishambulia Bajeti ya Upinzani kwa
maneno ambayo aliyasema anaweza kuyafananisha na uchizi.
“Wanasema
mipango, unafikia kusema maneno mengine ni ya uchizi uchizi, hivi
kutokana na maeneno yaliyotekelezwa, kama ya upinzani haitekelezeki,
lakini tumezungumza pensheni ya wazee katika bajeti iliyopita, kwa
bahati mbaya wabunge hawa wa CCM sijui hamuwasikilizi hata viongozi
wenu?" alihoji Mnyika.
Alifafanua kuwa ,"Suala la malipo ya
pensheni kwa wazee, hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwahi kulizungumza
mjini Morogoro katika sherehe za wazee, na aliahidi Serikali itakwenda
kutoa pensheni ya wazee. Sasa hapa unaposema haitekelezeki ndio maana
unafikia kusema kuna kauli nyingine kama ni za uchizi uchizi hivi."
Alisema
pia katika suala la ongezeko la mishahara hadi kufikia 315,000,
wamerudia katika bajeti ya upinzani kwani linawezekana, sitaki kutaja
hapa takwimu za wafanyakazi wote wa Serikali na malipo yao.
“Lakini,
bunge lililopita tulitoa takwimu hapa jinsi ambavyo inawezekana
mshahara kima cha chini ufikie 315,000 na ndio sababu leo tumerudia
tena, kwani Serikali haijatekeleza, lakini kuna wapofu wa kumbukumbu
ambao hawasomi kumbukumbu za bunge," alisema Mnyika.
Nje ya Bunge Baada
ya agizo hilo la Ndugai, askari wa bunge walimwondoa Mnyika na
kumsindikiza hadi nje ya uzio wa bunge, ambako alizungumza na wanahabari
na kufafanua kuwa, alisema Rais Kikwete ni dhaifu kutokana na sababu
ambazo alikuwa nazo, ila hakupata nafasi ya kuzitaja.
Alisema
sababu hizo zilitokana na bajeti ya Serikali ambayo ilisomwa bungeni,
ambayo haitekelezeki na inakinzana na Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Mpango
wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano.
“Bajeti hii ni matokeo ya
udhaifu wa Rais Kikwete, narudia tena kwani yeye ndiye aliyesaini
Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa nchi
tena kwa wino mwekundu, mpango ambao sasa unapingana na bajeti hii,”
alisema.
Alisema pia Rais Kikwete ni dhaifu kwani ndiye
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na bajeti ilipita katika baraza hilo,
lakini imedhihirika kwamba haikuzingatia kuzingatia mpango wa maendeleo,
pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya
udhaifu.
"Mnyika alisema pia kwa mujibu wa Katiba, Rais ndiye
anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba.
Hivyo Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti, hivyo Rais Kikwete
anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye Baraza la
Mawaziri ikafanyiwe marekebisho kama atataka," alisema.
Hata
hivyo, alisema kutokana na ubovu wa Katiba, michango ambayo inaendelea
sasa bungeni, haitaweza kupinga bajeti kwani inatakiwa ipitishwe kwa
kupiga kura kwa kila mbunge, na kama wabunge wengi wakipinga ina maana
Rais atalivunja bunge na hivyo kufanyika uchaguzi mwingine, kitu ambacho
wabunge wa CCM hawatakubali.
Nassari alia na wabunge wa CCM
Katika
hatua nyingine, kutokana na uamuzi huo wa kutolewa nje Mnyika, wabunge
kadhaa wa Chadema pia walitoka kwa hiari yao, akiwapo Mbunge wa Jimbo la
Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ambaye alisema wakati anagombea
ubunge hakudhani kuwa bunge kama chombo kikubwa cha uamuzi, chenye
umuhimu mkubwa kwa Watanzania hasa kipindi hiki cha kupitisha bajeti,
linaweza kutumiwa kama mkutano wa chama na kutupiana mipasho.
“Nimesikitika
sana nimeona ni bora nitoke, bunge limekuwa la mlengo wa kisiasa na
kupeana mipasho, nasikitika Mnyika kutolewa nje.
Alisema Mbunge
wa Mtera, Livingstone Lusinde alitoa kauli za kuudhi wapinzani, lakini
spika alimwambia arejee maneno yake mara ya pili,” alisema Nassari.
Kabla
ya Mnyika kutolewa nje, Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Mchungaji
Peter Msigwa, pia alionywa na Ndugai kutokana na kutoa kauli za kumpinga
pale alipomtaka Mnyika afute kauli yake.
“Naomba wananchi wa
Iringa mjini, kupitia Mchungaji Msigwa ni vizuri kuwa na nidhamu kwa
bunge hili. Hiki ni kikao kikubwa, anayezungumza ni Mnyika nimemkataza
kuita mtu chizi…, muache hii habari ya kuropoka kama una jambo simama,
kiti ndio kina uamuzi wa mwisho,” alisema Ndugai.
Pia Ndugai,
alikataa mwongozo wa Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje ambaye alitaka
mwongozo, kuhusiana na kauli za kuudhi ambazo zilitolewa juzi na Mwigulu
Nchemba (Iramba Magharibi.
Nchemba atuzwa Sh210,000 wa
Uchumi na Fedha wa CCM, juzi alituzwa Sh210,000 baada ya kuiponda bajeti
ya upinzani na kuiita ni ya kipuuzi na haitekelezeki, wapinzani wamejaa
uigizaji na kumrushia kombora Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman
Mbowe kuwa anawahadaa Watanzania kwa kukataa gari kuukuu, na baada ya ya
kupewa jipya alikubali kimya kimya.
Nchemba akizungumza na
waandishi nje ya bunge, alisema jumla ya fedha alizopewa na wabunge na
mawaziri kadhaa zilifikia Sh210,000. Mchango wa Lusinde
Mbunge wa Mtera-CCM, Livinstone Lusinde alisema bajeti ya upinzai ya uongo na haitekelezeki.
Lisinde
huku akieleza kumuunga mkono, Nchemba alisema yaliyoandikwa hayana
uhusiano na ilani ya uchaguzi wa Chadema, kwani waliwahi kusema watatoa
elimu bure lakini suala hilo halimo kwenye bajeti.
Kauli hiyo ya
Lusinde ilimfanya Naibu Spika kumtaka airejee tena, naye akarudia maneno
yake kuwa hutuba hiyo ya bajeti kivuli ya upinzani inatofautiana na
Ilani ya Uchaguzi ya Chadema kwani suala la elimu bure halipo.
Lusinde
pia alimrushia alisema Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani
bungeni, anajidai kukataa posho ya Sh80,000 lakini, anakubali malipo ya
Sh2 milioni kwa mwezi huku akitembelea gari la kifahari la Serikali. |
No comments:
Post a Comment