Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philiph Mpango akifurahia jambo na Bi. Bella
Bird ambaye ni Mkurugenzi Mkazi anayeiwakilisha Benki ya Dunia katika
nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia wakati wakisubiri kuingia
kwenye mkutano Jijini Washington DC.(Picha zote na Wizara ya Fedha na
Mipango)
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James akisalimiana na Bi.
Bella Bird ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anaewakilisha
benki hiyo katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia akiwa
pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Jijini
Washington DC.
Bi.
Bella Bird, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anaewakilisha Tanzania,
Burundi, Malawi na Somalia akifafanuliwa masuala mbalimbali ya Tanzania
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James (kulia)
pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango(katikati) Jijini
Washington DC.
Kaimu
Kamishna wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya
Nishati na Petroli Bw. James Andilile akimweleza Kaimu Kamishma wa Sera
Bw. Agustine Ollal (kushoto) na Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo
(kulia) kuhusu Tanesco inavyopiga hatua katika uimarishaji wa nishati
kwa wananchi, wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na IMF
unaoendelea Jijini Washington DC, Marekani.
Wajumbe
kutoka Tanzania waliohudhuria Mkutano wa Benki ya Dunia wakiwa kwenye
Mkutano wa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Jijini
Washigton DC.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akieleza ni jinsi gani Benki ya
Dunia inafurahia utendaji kazi wa nchi ya Tanzania hasa katika kukuza
uchumi, kulia kwake ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Natu
Mwamba anaemfuatia ni Bw. Johson Nyela Mkurugenzi wa Sera Uchumi na
Utafiti na Bw. Dickson Lema Meneja Masuala ya Fedha kutoka Benki Kuu ya
Tanzania Jijini Washgton DC, Marekani.
Makamu
wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar
Diop akifafanua masuala mbalimbali namna Benki hiyo ilivyojipanga
kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi yake mbalimbali
ya kipaumbele wakati wa mazungumzo kati ya Benki hiyo na Ujumbe kutoka
Tanzania unaohudhuria mkutano wa mwaka wa Benki hiyo na Shirika la Fedha
la Kimataifa-IFM, unaofanyika Washington DC nchini Marekani
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndullu akimweleza jambo Mkurugenzi
Msaidizi wa Benki ya Dunia ya Afrika Bw. Makhtar Diop (Hayupo pichani)
juu ya miradi mbalimbali ambayo Benki ya Dunia inaweza Kusaidia Tanzania
katika Sekta mbalimbali kwani kwa sasa uchumi wa Tanzania umekuwa kwa
kiasi cha kuridhisha kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango akifuatiwa na Waziri wa Fedha wa Zanzibar Dkt. Khalid
Salum Mohamed, Jijini Washington DC, Marekani
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndullu akimwonesha kitabu waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango walipokuwa kwenye mkutano na
Mkurugenzi Msaidizi wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Jijini Washigton
DC, Marekani.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akifurahia jambo na Mchumi Mkuu
wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bw. Albert Zeufack alipotoka kwenye
mkutano, Jijini Washigton DC, Marekani.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akifurahia jambo na Mchumi Mkuu
wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bw. Albert Zeufack alipotoka kwenye
mkutano, Jijini Washigton DC, Marekani.
........................................................
Benny Mwaipaja, MoFP-Washington DC
BENKI
ya Dunia inakusudia kuipatia Tanzania ruzuku na mkopo wenye masharti
nafuu wa dola Bilioni 1 nukta 6 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 3
nukta 5 kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo
nishati ya umeme, kilimo biashara na ukarabati wa miundombinu ya reli ya
kati.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu amesema Jijini Washington
DC, Marekani ambako Ujumbe wa wataalamu wa masuala ya uchumi na Fedha
kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanashiriki mkutano wa mwaka wa Benki
ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF kwamba mazungumzo kuhusu
mkopo huo yako katika hatua za mwisho.
Prof.
Ndulu amesema kuwa upatikanaji wa mkopo huo utaisaidia serikali
kuboresha miundombinu yake mbalimbali ili kuharakisha maendeleo ya sekta
ya viwanda kwa kuimarisha pia mazingira ya sekta binafsi
kufanyabiashara na kuwekeza mitaji na teknolojia.
“Mbali
na mkopo huo ambao ni muhimu kwa taifa, tunajadili pia namna ukuaji wa
uchumi unavyotakiwa kuakisi maisha ya kawaida ya wananchi wetu kwa
kupiga hatua kimaisha na kuondokana na umasikini” alisema Gavana Prof.
Ndulu.
Aidha,
amesema kuwa Benki ya Dunia imesifu hatua zilizofikiwa na serikali ya
Tanzania katika kukuza na kusimamia uchumi wake ambao licha ya uchumi wa
dunia kushuka viwango vyake vya ukuaji uliotarajiwa wa asilimia 3.3 na
kukua kwa asilimia 1.5 tu, Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi ya
asilimia 7.
“Tanzania
ni miongoni mwa nchi nne zinazoendelea ambazo uchumi wake unakua kwa
kasi na unatarajia kukua zaidi kutokana na kuvumbuliwa kwa gesi na
kushuka kwa mfumuko wa bei” Alisisitiza Prof Ndulu
Kiongozi
wa ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo, Waziri wa Fedha na Mipango,
Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa mkopo utakao tolewa ni pamoja na dola
milioni mia 2 kwaajili ya kulijengea uwezo shirika la ugavi wa umeme
nchini Tanzania-Tanesco ili liondokane na nakisi inayosababishwa na
madeni makubwa yanayolikabili shirika hilo
Dkt.
Mpango Amefafanua kuwa mkopo huo pia utaiwezesha serikali kulipa madeni
inayodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii baada ya kufanyika kwa uhakiki
wa kina wa madeni hayo ili kuiwezesha mifuko hiyo itoe huduma
inayostahili kwa wananchama wake.
Amesema
kuwa kiasi kingine cha fedha hizo kitatumika kuijengea uwezo sekta
binafsi iweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa Taifa pamoja na
kuimarisha kilimo kwa kuwawezesha wakulima kulima kilimo cha kibiashara
na kuondoa kodi zenye kuleta kero katika sekta ya kilimo.
“Wakati
tunatekeleza mpango huo tutaangalia pia namna ya kupitia upya kodi
zinazolalamikiwa katika sekta ya utalii” amefafanua Dkt. Mpango
Kwa
upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Dkt. Khalid Mohamed, ameishukuru Benki ya dunia kwa kuisaidia
nchi hiyo kupitia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa visiwani
humo ikiwemo uboreshaji wa rasilimali watu, miundombinu ya barabara,
kiwanja cha ndege na kuboresha mazingira yatakayochangia kukua kwa sekta
ya utalii visiwani humo.
Makamu
wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Makhtar
Diop, amesema kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali ya
Tanzania ili iweze kufanikiwa kiuchumi na kijamii.
Amesifu
juhudi na hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya Tano
inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli kwa kurejesha nidhamu ya kazi
na kupambana na vitendo vya ufisadi hatua ambayo inaungwa mkono na benki
yake ili kuharakisha maendeleo ya nchi na wananchi wake kwa ujumla.
Diop
amebainisha kuwa Benki yake inataka kuona Shirika la Umeme Tanzania
Tanesco linaboreshwa na kuwa la kisasa kwakuwa nishati ni nyenzo muhimu
ya kukuza uchumi wa viwanda na kwamba wangependa kusaidia eneo hilo
namengine ya kuboresha rasilimali watu kwa kuwekeza kwenye elimu na
kuwainua wananchi kimapato kupitia mradi wa TASAF na mingine
itakayoanzishwa.
No comments:
Post a Comment