RAMBIRAMBI MSIBA WA MTANGAZAJI JOSEPH MAPUNDA
Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha
mtangazaji wa michezo wa Radio Wapo, Joseph Mapunda kilichotokea jana
asubuhi (Julai 21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Msiba
huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa
nyakati tofauti Mapunda alifanya kazi na TFF kwa kuripoti shughuli zetu
nyingi za mpira wa miguu, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF
inatoa pole kwa familia ya marehemu Mapunda, Radio Wapo na Chama cha
Waandishi wa Habari Tanzania (TASWA) na kuwataka kuwa na subira na
uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA DOREFA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) uliochaguliwa katika
uchaguzi uliofanyika jana (Julai 21 mwaka huu).
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa DOREFA walivyo na imani kubwa kwao katika
kusimamia mchezo huo mkoani Dodoma.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya DOREFA
chini ya uenyekiti wa Nasoro Kipenzi ambaye amechaguliwa kwa kipindi cha
pili mfululizo.
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha
shughuli za mpira wa miguu mkoani Dodoma kwa kuzingatia katiba ya DOREFA
pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya DOREFA na Kamati ya Uchaguzi
ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za
uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliofanyika hoteli ya Dear Mama ni
Nassoro Kipenzi (Mwenyekiti), Thadeo Kaliza (Makamu Mwenyekiti), Stewart
Masima (Katibu Mkuu), Kepha Maswaga (Mhazini), Mulamu Ngh’ambi (Mjumbe
wa Mkutano Mkuu TFF), Mohamed Aden (Mwakilishi wa Klabu TFF), Zawdi
Kassim (Mjumbe Kamati ya Utendaji).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment