Friday, October 7, 2016

WAZIRI NAPE NA WAREMBO WA MISS TANZANIA MKOANI DODOMA


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo MHE. Nape Nnauye akizungumza na vyombo vya habari leo katika Hotel ya Morena Dodoma baada ya kuzungumza na washiriki 30 wa Fainal za shindano la Miss Tanzania 2016. Kushoto ni Miss Dodoma Anna Nitwa, ambaye ni mwenyeji wa washiriki wote. 
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), Profesa Ammi akizungumza na washiriki wa fainali za Miss Tanzania 2016, waliotembelea chuoni hapo leo kwa shughuli za kijamii za kupanda miti katika eneo la chuo hicho. 
Baadhi ya washiriki wa fainal za Miss Tanzania 2016, Spora Luhende kutoka Kanda ya Ilala na Siah Pius kutoka Kanda ya Kinondoni, wakishiriki katika zoezi la kupanda miti leo katika eneo la Chuo KIkuu cha Dodoma.
Washiriki wa fainali za Miss Tanzania Noor Kondo Miss Ukonga 2016 kutoka Kanda ya Ilala wakishiriki katika zoezi la kupanda miti katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo 6 Okt 2016.

No comments:

Post a Comment