Marekani imechukizwa na kitendo cha mahakama moja nchini
Pakistani kumuhukumu adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela, tabibu
aliyetumika kuisaidia CIA kujulikana alipo Osama bin Laden.
Richard Durbin ambaye ni miongoni mwa maseneta wa taifa hilo amesema kitendo cha uamuzi huo wa kupunguza msaada, ulioungwa mkono kwa kura 30 na hakukuwa na kura hata moja iliyopinga, kinaonyesha namna walivyochukizwa na kifungo kwa dakitari huyo.
Uamuzi wa kamati hiyo ya matumizi umefikia maamuzi haya baada ya kamati ndogo kuitadhalisha Pakistan kuwa Marekani inaweza kupunguza misaada kwa taifa hilo ikiwa halitafungua njia kwa majeshi ya NATO katika nchi jirani na Afghanistan.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillay Clinton alisema hakukuwa na sababu za msingi kwa Pakistan Kumfunga Daktari Afridi na kaapa Marekani itahakisha suala hili kuigharimu Pakistan.
" Marekani haikubaliani na misingi ya hukumu hii ya Dakitari Afridi kwani msaada wake ulikuwa mkubwa kwa kupatikana kwa muhalifu mkubwa duniani."
Dakitari Shafidi alituhumiwa kwa kutoa chanjo za uongo katika kampeni ya chanjo ambayo ilisaidia kupata taarifa za kinasaba kumhusu Osama Bin Laden na familia yake na inaaminika ziliisaidia mno idara ya upelelezi ya Marekani FBI na ile ya ujasusi CIA , kujua mahala alipo Osama Bin Laden.
Kiongozi huyo wa zamani wa Al-Qaeda aliuwawa katika mji wa Abbottabad mwaka mmoja uliopita na kikosi maalumu cha Marekani. Tangu kulipotokea tukio hilo kumekuwa na shutuma nyingi kwa Pakistan kutoka Marekani. Huku baadhi ya Wamarekani wakilitaka taifa lao kuinyima misaada nchi hiyo.
Kwa muda sasa Pakistan imekuwa miongoni mwa mataifa yanayopokea msaada mkubwa kutoka Marekani .
No comments:
Post a Comment