Friday, May 25, 2012

JOSEPH SELASINI MBUNGE WA ROMBO APATA AJALI MBAYA MAMA YAKE AFARIKI KATIKA AJALI HIYO

Mbunge wa Rombo akifafanua jambo
Mbunge Mbunge wa Rombo, Mhe. Joseph Selasini amepata ajali mbaya  sana wakati alipokuwa akiendesha gari lake mkoani Kilimanjaro, ambapo watu 3 kati ya watu 6 waliokuwemo kwenye gari hilo wamepoteza maisha na miili yao imechukuliwa na gari la polisi na  kupelekwa hospitali ya KCMC Moshi kutoka Boma Ng'ombe.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro  Absalom Mwakyoma amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo akielezea zaidi amesemailikuwa ni saa 1:00 jioni maeneo ya Boma Ng;ombe ambapo Mh Joseph Selasini wakati akiendesha gari hilo akitokea Arusha,  ghafla aliona mwendesha Pikipiki wakati akijaribu kumkwepa ndipo gari lake likapinduka.

 Watu wengine akiwemo mbunge huyo na mke wake alifahamika kwa jina la Digna Kavishe waliojeruhiwa katika ajali hiyo, wako katika hospitali ya Boma Ng'ombe  hali zao zinaendelea vizuri na muda mfupi nao watapelekwa katika hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi pia katika watu aliokuwa nao ni pamoja na mama mzazi wa muheshimiwa ambae inasemekana kuwa amefariki dunia katika ajali hiyo

Ajali hiyo imetokea majira ya saa moja jioni ikilihusisha gari lake aina ya Toyota, Land Cruiser lenye namba za usajili T441DRT alilokuwa akiliendesha mwenyewe.

Chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa kuwa kimetokana na jitihada za kukwepa kungonga mwendesha pikipiki, ndipo gari lilikosa mwelekeo na kupinduka.

Ndani ya gari walikuwemo watu sita, ambapo watatu wamepoteza uhai akiwemo Mama Mzazi, Grace Shao na shangaziye Mbunge huyo. Waatatu waliosalia akiwemo Baba Mzazi na mtu mwingine walikuwa wamejifunga mikanda na kusalimika.

Hali ya Mhe. Silasini  inaelezwa kuwa "ni nzuri" (SI mahututi) amejeruhiwa mkono. Yeye pamoja na majeruhi wengine walioumia vibaya

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi.

No comments:

Post a Comment