Tuesday, May 15, 2012

MADUKA 10 YATEKETEA KWA MOTO HUKO NGARAMTONI JIJIN I ARUSHA



 wananchi wakiwa wanasaidiana na askari wa zima moto kuzima moto huo
 wakati mungine iliwabidi watumie nguvu kubwa
 wananchi wakishuhudia zima moto wakizima wakifanya kazi hiyo
mdada akilinda vitu ambavyo amebahatika kuvitoa katika duka alilokuwa akifanyia kazi

Maduka 10 yenye thamani ya zaidi ya million 100 yameteketea kwa moto katika mji mdogo wa Ngaramtoni wilayaya Arusha vijijini ambapo chanzo halisi ni hitilafu ya Umeme.
 
Akiongea na Libeneke la kaskazini katika eneo la Ngaramtoni mmiliki wa maduka hayo Benjamini Mbayi alisema kuwa moto huo ulianza majaiara ya saa saba za mchana ambapo ulianza katika duka moja.
 
Alisema kuwa wakati moto huo unaanza alilazimika kuingia kwenye chumba hicho na kuzima umeme katika kiunganishi cha umeme (SOCKET) lakini bado haikusaidia kabisa na moto huo uliendelea kutapakaa katikia vyumba vingine vya biashara.
 
“Baada ya kuona moshi ukiwa unatapakaa kwenye paa ambapo kwa kweli nilishindwa kuokoa kitu chochote ila nilifanya jitiada za kuhakikisha kuwa tunaomba msaada hasa kwa kikosi cha zima moto jambo ambalo lilifanikiwa ndani ya dakika 30”alisema Mbayi.
 
Pia aliongeza kuwa mara baada ya hapo kikosi hicho kilifanikiwa kuzima moto lakini vitu venye thamani ya Milioni 100 vilikuwa vimeshateketea kwa Moto lakini kutokana na zoezi hilo la uokoaji hapakuwa na madhara yoyote yale ya kuunguwa kwa binadamu


Diwani wa kata ya Olmotony David Kinisi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa kutokea kwa matukio hayo ya mara kwa mara ya moto katika mji mdogo wa Ngaramtoni kunatokana na ubovu wa mundombinu hasa ya maeneo ya biashara hali ambayo kila mara inasababisha matatizo makubwa sana.
 
Kinisi alifafanua kuwa tukio la Moto katika mji huo wa Ngaramtoni ni la Pili ambapo mwezi uliopita maduka tisa nayo yaliteketea kwa moto huku maduka hayo yakiwa na gharama ya milioni 200 huku moja ya maduka yakiwa ni mali yake


”kama mnavyoona hapa ubovu wa miundo mbinu unachangia kwa kiwango kikubwa sana na kama halmashauri haoitaweza kuliangalia suala hili kwa undani zaidi basi itakuwa ni hatari sana kwani kuuungua kwa maduka haya ni dalili kubwa snaa ya umaskini hasa Ngaramtoni”alisema Kinisi.
 
Alifafanua kuwa hali hiyo inatakiwa kuboreshwa sana hasa katika eneo la Umeme kwa kuwa ndio chanzo kikubwa Sana cha kutokea kwa majanga ya moto kwa kuwa hata maeneo yaliongua ndio chanzo kikubwa sana cha hasara na umaskini katika mji mdogo wa Ngaramtoni.
 
Awali aliwataka wananchi hasa wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanafanya biashara kwa kuzingatia utaalamu wa mafundi wa umeme na wala sio kwa kuwatumia mafundi wa uchochoroni ambao ndio chanzo kikubwa cha majanga ya Moto.
 
Naye kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Thobias Andengenye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kujua thamani halisi ya maduka yaliyoangua katika janga hilo.
 
 
Source: http://www.woindeshizza.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment