Monday, May 28, 2012

Mazishi ya mpinzani wa Mafia yafanyika

Rais wa Italia, Giorgio Napolitano, amehudhuria mazishi ya kitaifa katika mji wa Sicilian ulioko Corleone ya kiongozi wa shirikisho ambaye aliuawa na kundi la Mafia zaidi ya miaka sitini iliyopita

Mtu huyo, Placido Rizzotto, aliwahamasisha wafanyakazi wa mashamba katika kupambana na Mafia kuhusu umiliki wa ardhi.

Alitoweka Machi 1948 na baadaye alipatikana akiwa amekufa mita kadhaa nje ya Corleone.
Baada ya miaka kampeni za familia yake na marafiki, Italia imempa heshma ya kupinga Umafia katika moja ya ngome zake.

Mji wa Corleone baadaye ulikosa umaarufu wa kuwa makazi ya familia za magenge ya kufikirika katika filamu ya Hollywood Godfather

No comments:

Post a Comment