Wednesday, May 16, 2012

MTOTO MCHANGA WA MWEZI MOJA NA SIKU TATU ARAFA HAJI SILIMA AMEUWA KIKATILI BADA YA KUKATWA PUA NA MASHAVU HUKO WESHA KATIKA WILAYA CHAKE CHAKE.


Kichanga cha mwezi moja na siku tatu cha jinsia ya kike cha nyofoliwa pua na kufariki dunia huko wesha katika wilaya chake chake huku akiwa amelala nyumbani kwao majira ya saa nne nanusu asubuhi ya siku ya jana.

Mara baada ya kunyofolewa pua kichanga huyo alitekelezwa barazani mbali na nyumbani kwao ambapo naibu sheha alimkuta na kutoa tarifa kwa wauguzi wa kituo cha afya ilikumpatia matibabu mtoto huyo. 

Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa Kusini Pemba Mohamed Shekhani Mohamed amemtaja mtoto huyo mchanga  kuwa ni Arafa Haji Silima mwenye umri wa mwezi moja na siku tatu.
Mkuu huyo wa pelelezi alisema uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea kufanywa na kuahidi kutoa tarifa kwa vyombo vya habari kila hatua itakayo fikiwa ikiwa pamoja na kuwapeleka mahakamani.

Alisema kuwa kufuatia tukio hilo , Jeshi la Polisi tayari linawashikilia Babu, bibi na mama wa kichanga hicho ambapo majina yao yalihifadhiwa kwasababu za kiuchunguzi.

Naye mama wa kichanga hicho ambae ni mama wa watoto pacha alieleza kuwa yeye alikuwa nje wakati huo akimnonyesha mtoto mwengine ndipo alipo ingia ndani kumueka ili amchukue mwengine amnyonyeshe hakuamini alipo ona sehemu yote ya pua haipo.

Muuguzi wa watoto katika kituo cha Afya Wesha Khadija Suleiman Omar alisema alipokea tarifa kutoka kwa naibu sheha wa Shehia ya Wesha Haji Mohamed Ali aliyemtaka aende nyumbani kwao mtoto huyo ambaye alihujumiwa pua alichukua vifaa vya huduma ya kwanza na kukimbia alipofika kwenye nyumba moja mbali na nyumbani kwao kichanga hicho alikikuta kikiwa kimetelekezwa barazani kimekwisha fariki Dunia .

Naibu sheha washehia ya wesha haji mohamed ali amesema mara baada kupokea tukio hilo aliliripoti kituo cha afya kuwaombea matibabu ila muuguzi alipo fika na kumuangalia alikuta tayri amekwisha fariki na kupiga tarifa polisi wakati

Mashavu mwalimu bilali 37 mkaazi wa wesha amesema hilo ni tukio  la pili kutokea katika kijiji hicho mwaka uliopita mtoto mwenye umri kama huo katika familia hio alikatwa kitovu na kufariki akipatiwa matibabu.

habari na
Hassan Ninga

No comments:

Post a Comment