Mbunge wa Jimbo la Monduli Edward
Lowassa akizungumza na wananchi (wafugaji) wa Kijiji cha Nararami Kata
ya Meserani, kwa muda mrefu wafugaji hao wamekuwa na mvutano na
mwekezaji wa shamba Abraham. Mgorogo huo umetajwa kuwa kwenye shamba
lenye Hekari 4,100 ambazo zipo ndani ya chanzo cha maji kinachotumika
wakati wa kiangazi kunyweshea mifugo na malisho.
Mwekezaji akiwa kwenye mkutano wa
usuluhisho uliokuwa ukiongozwa na Mbunge Edward Lowassa, hatata hivyo
baadhi ya wafugaji hao wa Kimaasai waligoma kukaa karibu na mwekezaji
huyo wakidai amekuwa akiwanyanyasa na kuua mifugo yao, pembeni yake ni
kijana wa Kimaasai akiwa ameusimika mkuki wake chini huku kikao
kikiendelea.
Baadhi ya watu wakiwamo akina mama wa
kabila la Wamaasai wakimpongeza Edward Lowassa kwa hatua ya kumaliza
mgogoro huo baada ya kupendekeza mwekezaji huyo atafutiwe eneo jingine
la kulima na eneo lenye chanzo cha maji alirudishe kwenye serikali ya
Kijiji.
Baadhi ya wafugaji wa Kimaasai wakiwa
wamepanda gari la Mwekezaji Abraham ambaye kwenye kikao walikuwa wakidai
hawataki hata kumuona kijijini hapo kutokana na kuua mifugo yao kwa
madai kuwa aliweka sumu kwenye majani.
No comments:
Post a Comment