Wednesday, May 23, 2012

RAIYA WA KENYA AKUTWA AMEFARIKI DUNIA NDANI YA CHUMBA CHA KULALA WAGENI

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Rick Musya Kalonzo raiya wa kenya amekututwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Stereo.
 Akizungumzi tukio hilo kamanda wa polisi mkoawa Arusha Thobias Andengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea may 19 mwaka huu majira ya saa 1:30 asubuhi maeneo ya kijinge ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Stereo . 
 Alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa za awali zinadai kuwa mtu huyo alifika katika nyumba hiyo majira ya saa 6:10 usiku na kujiandikisha kwenye kitabu cha wageni kwa jina la Kassim na kisha kupewa chumba no 2 wakati siku hiyo hiyo muda wa saa 1:30 asubuhi mmoja wa wahudumu alikwend kumgongea lakini aliposhika kitasa akakuta mlango unafunguka . 
 Alisema kuwa ndipo muhudumu akaingia ndani na kumkuta mteja wake akiwa aelala huku akiwa na matapishi yaliyotapakaa kitandani baada ya kuona hali hiyo aliamua kutoa taarifa katikakituo kikuu cha polisi ambapo mara baada ya kupata taarifa hiyo baadhbi ya askari walikwenda kwenye eneo la tukio na kuukutamwili huo .
 "sasa kufuatia hali hiyo polisi waliofika eneo lile waliamua kufanya uchunguzi na kugundua kwamba inawezekana kifo chake kilisababishwa na unywaji wa sumu kwani iligunulikka kulikuwa na chupa ya sumu aina ya Twigartaz stock spray ambayo ilikuwa imetupwa nje ya dirisha la chumba laichokuwa amelala na pia mara baada ya kupekuwa begi lake walikuta kamba ya manila na hati ya kusafiria ambayo ilikuwa imechanwa chanwa na baada ya kuunganisha ikasomeka kuwa ni hati ya kusafiria No.Boo3503198D na jina liliandikwa ni Rick Musya Kalonzo iliyoonyesha kazaliwa tarehe 1/10/1957 katika kijiji cha Tungutu katika tarafa ya Changwitya,wilaya ya kitui mkoa wa kati"

alifafanua Adengenye Alisema kuwa hatua zaidi kuhusiana na upelelezi wa kifo hicho unaenelea na mwili wa marehemu umeifadhiwaktika hospiatali ya mkoa ya Mounti Meru kwa ajili ya uchunguzi wa kidaktari.

No comments:

Post a Comment