Sunday, May 27, 2012

Wacongo wakimbilia Uganda na Rwanda



Taarifa kutoka Jamhuri ya Demokrasi ya Congo zinaeleza kuwa mapigano yanaendelea mashariki mwa nchi baina ya wanajeshi wa serikali na wanajeshi walioasi.
Mfanyakazi wa Msalaba Mwekundu amsaidia mtoto mashariki mwa DRC
Msemaji wa waasi, Vianney Kazarama, aliliambia shirika la habari la Ufaransa, kwamba jeshi la serikali linashambulia kituo chao kimoja kwa silaha nzito, huko Kivu-Kaskazini.
Mapigano hayo yalianza kama siku 10 zilizopita.

Umoja wa Mataifa unasema maelfu ya watu wamekimbia ghasia hizo, wengi wao wameelekea Uganda na Rwanda.

Waasi hao wanasema wao wamo kwenye vuguvugu la March 23, ambalo asili yake ni kundi la wapiganaji wa Kitutsi, la CNDP.

Walikubali kujumuika na jeshi la Congo, lakini sasa wanadai kuwa wanataka makubaliano ya amani ya mwaka wa 2009 yatekelezwe kikamilifu.

No comments:

Post a Comment