Saturday, June 23, 2012

Ajali ya lori, daladala yaua watatu, kujeruhi wanane Dar

Wapita njia wakiangalia basi la daladala lililogongwa na lori eneo la Tegeta Kibaoni, jijini Dar es Salaam jana. Watu wawili walikufa kwa kugongwa na lori hilo na abiria wanane wa basi
 
Watu watatu wamefariki dunia na wengine nane kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyohusisha lori na daladala katika eneo la njia panda ya Wazo na Tegeta, jijini Dar es Salaam.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela, alisema ajali hiyo ilitokea jana asubuhi baada ya lori kuligonga daladala lililokuwa limeegeshwa ambapo pia sehemu baa ya KMKM pamoja na duka vilibomolewa.

Aliwataja waliofariki kuwa ni Halima Msoro (35- 40) aliyekuwa mamalishe katika baa hiyo na mwanaume mpita njia, ambaye jina lake halikufahamika mara moja.
Habari zilizopatikana wakati tukienda mitamboni, zinaeleza kuwa mtu mwingine wa tatu alifariki dunia njiani wakati akipelekwa hospitali. Hata hivyo, zilikanushwa na Kamanda Kenyela.
Kenyela alisema chanzo cha ajali hiyo ni kufeli kwa breki za lori aina ya tipper Scania, lililokuwa likitokea katika Kiwanda cha Saruji cha Wazo, na hivyo kuvamia daladala hilo hilo aina ya Isuzu Journey linalofanya safari Kariakoo- Tegeta, lililokuwa linapakia abiria sehemu, ambayo hairuhusiwi.
Kenyela alisema majeruhi, walipelekwa katika Hospitali ya Mwananyamala.


hapo chini ni baadhi ya picha za tukio hilo la ajali



Wananchi wa eneo la Tegeta Kibaoni, jijini Dar es Salaam wakisaidiani na polisi kuupakiza mwili wa mmoja wa mwananchi kwenye gari kati ya watu waliokufa katika  ajali iliyotokea baada ya Lori la mchanga kupata hitilafu ya breki  na kuacha  barabara na kugonga Daladala kabla ya kuvamia baa na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo na wengine nane kujeruhiwa leo.Picha kwa hisani ya MOBILE STUDIO 2002.

Wananchi wa eneo la Tegeta Kibaoni, jijini Dar es Salaam wakijaribu kutoa mwili wa mmoja wa mwananchi kati ya watu waliokufa katika  ajali iliyotokea baada ya Lori la mchanga kupata hitilafu ya breki  na kuacha  barabara na kugonga Daladala kabla ya kuvamia baa na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo na wengine nane kujeruhiwa leo.Picha kwa hisani ya MOBILE STUDIO 2002.


No comments:

Post a Comment