Wednesday, June 27, 2012

Ajinyonga kwa kulea watoto wasiokuwa wa kwake


Mtu mmoja Silvester Prosper (44), amejinyonga kwa sababu ya kuambiwa analea watoto wawili wasio wakwake.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Charles Kenyela, alisema tukio hilo lilitokea Juni 24 mwaka huu, majira ya saa 3:00 maeneo ya Kinondoni Gundula.

Kamanda Kenyela alisema hivyo Silvester alijinyonga kwa kutumia kamba ya katani ambayo aliifunga chumbami kwake juu ya kenchi.
Hata hivyo, kamanda Kenyela alisema kwamba marehemu aliacha ujumbe uliokuwa ukisema “nimechoshwa na maisha ya Duniani, sistahili kuwepo hasa kwa mke wangu aitwaye Christina Kilahilo (32) mkazi wa Kinondoni kwa kisa cha kuniambia watoto alionao siyo wangu.”

No comments:

Post a Comment