Kamanda wa polisi mkoani Manyara Akili Mpwapwa
MCHIMBAJI mdogo wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilaya
ya Simanjiro Mkoani Manyara amenusurika kuuawa na wakazi wa mji huo
kwa madai ya kumtumia mtoto wake kwa imani za ushirikina ili apate
madini hayo.
Hali hiyo ilijitokeza jana saa 5 asubuhi baada ya askari polisi wa
kituo cha Mirerani kumfikisha kwenye nyumba anayoishi mchimbaji huyo
kwa ajili ya kufanya upekuzi wa kuchukua vifaa alivyokuwa anampigia
mtoto wake.
Kamanda wa polisi mkoani Manyara Akili Mpwapwa alisema mchimbaji
huyo,Antony Bedan (25) mkazi wa Zaire mji mdogo wa Mirerani
anashikiliwa na polisi kwa kosa la shambuli la kudhuru mwili mtoto
wake.
Kamanda Mpwapwa alisema Bedan anatuhumiwa kumjeruhi mtoto wake Monica
Bedan (3) sehemu tofauti mwilini mwake ikiwemo kichwani,usoni,juu ya
kiganja cha mkono na mgongoni.
Alisema Bedan anatuhumiwa kumpiga mtoto wake Monica kila wakati kwa
muda mrefu na wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya
kumfikisha mtoto huyo mahakamani.
Hata hivyo,wakiongea na waandishi wa habari baadhi ya wakazi wa mji
huo walidai kuwa Bedan anajihusisha na imani za ushirikina kwani huwa
anamlaza mtoto wake kwenye uvungu wa kitanda kama wafanyavyo misukule.
Walisema mchimbaji huyo alikwenda kwa waganga na akaambiwa awe
anampiga mtoto wake Monica kasha damu ikitoka ajipake usoni ndipo
atapata madini ya Tanzanite kwenye mgodi mmoja uliopo kitalu D (jina
tunalo).
Watu hao walitaka kumuua mama wa mtoto huyo Anjelina Theopil (26)
wakimtuhumu anashirikiana na Bedan kumfanyia vitendo vya kishirikina
mtoto wao lakini aliokolewa na polisi kwa kuhamishwa kwenye mji huo.
Theopil mwenye watoto wanne alisema Bedan alikuwa anampiga mtoto wao
Christina (5) na kumning’iniza kichwa chini miguu juu ili atoke damu
puani na kumwagia mtoto wao Monica ili apate madini ya Tanzanite.
Kwa siku ya jana kundi kubwa la watu wa mji mdogo wa Mirerani lilifika
kwa wingi kwenye kituo cha polisi kumshuhudia mtuhumiwa huyo huku
wengine wakiomba watolewe ili wamuue lakini polisi waliweza kudhibiti
kitendo hicho.
Hata hivyo,akizungumza kwa masikitiko wakati akirudishwa kwenye kituo
hicho cha polisi Mirerani Bedan aliiomba jamii imsamehe kutokana na
yeye kufanya kitendo hicho cha kikatili kwa mtoto wake mwenyewe.

No comments:
Post a Comment