serikali mkoani
kilimanjaro inakamilisha zoezi la kuwabaini watoto wote wanaoishi katika
mazingira hatarishi,hatua ambayo itasaidia kuzifahamu familia zenye
uwezo lakini bila ya sababu ya msingi zimeshindwa kuwajibika katika
maisha ya kila siku ya watoto wanaowahusu.
mkakati huo wa serikali mkoani kilimanjaro umetolewa na mkuu wa wilaya ya hai mhe novatus makunga wakati akimwakilisha mkuu wa mkoa wa kilimanjaro mhe leonidas gama katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika ambapo kwa mkoa wa kilimanjaro yalifanyika katika wilaya ya siha.
mhe makunga ameeleza kuwa mkakati huo unachukuliwa wakati serikali ipo katika kukamisha mchakato wa sera ya taifa ya malezi,makuzi na ustawi wa watoto.
amesema kuwa sera hiyo itaweka bayana haki ya mtoto na kuwa na sheria ambayo itasaidia makuzi na malezi ya mtototo
amefafanua pia itasaidi kuwabana wazazi wote ili wawawjibike katika maisha ya kila siku ya mtoto.
akizungumzia hali ya mkoa wa kilimanjaro,mhe makunga ameeleza kuwa una watoto wapatao 29,000 wanaoishi katika mazingira hatarishi kutokana na utambuzi uliofanywa katika halmashurii za wilaya za siha,hai na same na katika kata tatu za halmashauri ya moshi vijijini.
Mhe Makunga ameeleza kuwa utambuzi huo utakamilishwa katika wilaya zilizobaki za rombo,mwanga na manispaa ya moshi na katika kata 28 zilizobaki za moshi vijijini.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya siha Dk Charles Mlingwa ameeleza kuwa serikali katika wilaya hizom umeweka mtandao wa ushiorikiano unaolenga kuinua kipato cha wananchi ili waweze kuwa na nuwezo wa kuzihudumia kaya zao hususani watoto kwa mahitaji yote muhimu

No comments:
Post a Comment