BARAZA kuu la waislam nchini, BAKWATA, Mkoa wa Arusha, limemtaka
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la
Kirutheri KKKT Dayosisi ya mkoani
Arusha,Thomas Lazier, kuthibitisha madai
yake aliyoyatoa hivi karibuni katika Vyombo vya habari ya kuwepo Vijana zaidi ya 300 wanaofanya
mazoezi kwa ajili ya kuchoma makanisa na kuharibu mali mbalimbali
zinazomilikiwa na makanisa mkoani Arusha
vinginevyo Bakwata, itachukua hatua zinazostahili dhidi ya madai hayo.
Kauli hiyo imetolewa na Shekh, wa Bakwata Mkoa wa Arusha,
Shaaba Juma,alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kufuatia taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari hivi karibuni zikimnukuu
AskofuThomas Laizer, wa KKKT, akiwatuhumu
Vijana zaidi ya 300, wa kiislam kuwa wanakusanyika kila siku na kufanya mazoezi ya Karate,kwa kujiandaa
kuchoma na kuharibu makanisa mkoani
Arusha.
Shekh, Shaaban amesema Bakwata imeshitushwa na taarifa hizo
za kuwepo kundi laVijana 300 wa kiislam,wanaofanya mazoezi ya Karate, katika
msikiti ambao hakuutaja jina lake aliodai kuwa upo katika Eneo la Unga limited jijini Arusha, wanaofanya mazoezi
kwa ajili ya kuchoma makanisa na kuharibi
mali mbaklimbali zinazomilikiwa na
makanisa..
Alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa hiyo ya
kusikitisha, aliitisha kikao na Mashekh
, Maimam na walimu wa madrasa katika kata ya Unga limited ambapo viongozi hao
walisikitishwa na taarifa hiyo ambayo walisema haina ukweli wowote na kama
Askofu huyo anao ushahidi wakamtaka
kutoa taarifa hiyo kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama ili ifanyiwe
kazi.
Shekh Shaaban, alisema kuwa amewasiliana na mkuu wa mkoa wa
Arusha, Magesa Mulongo, ambae wamekubaliana
kukutana siku ya Jumatano Julai 13 mwaka huu ili Askofu, huyo aweze kutoa ufafanuzi wa
madai yake hayo mbele ya viongozi wa Dini na Serikali ili kupata ukweli wa madai hayo .
“Mimi Shekh wa mkoa sina taarifa hizo ninaona taarifa hii
ni ya hatari, inayolenga kuchafua Uislam na Waisam, nimefuatilia sijaona ukweli wowote kuhusu madai hayo, Kauli ya Askofu haifai kupuuzwa hata kidogo kwa sababu
imetolewa na kiongozi mkubwa wa Kanisa” alisema Shehk shaaban
.
Shekh, shaaban, alisisitiza kwamba hakuna msikiti wenye Vijana 300 kama
inavyodaiwa na Askofu huyo, wanaofanya mazoezi
ya Karate,kwa ajili ya kuyachoma moto makanisa,na kufanya uharibifu wa
mali kauli hiyo inalenga kuchonganisha
Waislam na Wakiristo na serikali yao na hivyo kujenga Taswira mbaya dhidi ya Dini Kiislam .
Akasisitiza kuwa Waislam na wasiokuwa waislam siku zote
wameishi kama ndugu hivyo kauli hiyo isitumike kujenga fitina ya kuwagombanisha wananchi na kuvuruga amani na
utulivu uliopo hapa nchini ambao umedumu kwa miaka mingi kwa kutambua kuwa kila
mmoja ana uhuru wa kuabudu dini aitakayo.hivyo kama anazo taarifa sahihi
aziwasilishe kwenye vyombo vya dola alisisitiza shehkh Shaaban.
Hivi karibuni magazeti ya Habari leo la juni 4 na An –Nuur
ya Ijumaa Juni 8 yenye vichwa vya habari
tofauti yalimnukuu Askofu Laizer,ambapo gazeti la Habari leo liliandika Uamsho
waibukia Dar es Salaam, wakati gazeti la An –Nuur ,likiandika Askofu Laizer,
anawajua waliochoma moto makanisa hata
hivyo baadhi ya viongozi wa makanisa
wakiwemo mapadri, wamesema madai ya
Askofu huyo yatapelekea kuwachonganisha waislam na dini zingne i kwa
kuwa hakuifanyia utafiti
No comments:
Post a Comment