AFISA kwa shule za msingi katika Halmashauri ya Manispaa ya
Arusha Bw Omary Mkombole amesema kuwa katika msimu wa Mithiani ya mwaka 2012
shule yeyote ambayo itaonekana kuwa na kasoro za majibu ya mithiani basi
atalazimika kushinikiza shule hizo zifutiwe usajili wa kudumu
Alitoa Kauli hiyo mjini Arusha wakati akifungua mkutano
baina ya wamiliki na mameneja wa shule binafsi kwa mkoa wa Arusha (TAMONGSCO)mapema
wiki iliyopita.
Mkombole alisema kuwa haina tija kabisa kwa Shule ambazo
zinadanganya matokeo kuendelea kuwepo kwa kuwa hali hiyo ndiyo inayochangia kwa kiwango
kikubwa sana
kuongeza hata idadi ya wasiojua kusoma na kuandika ndani ya Taifa.
Alisema kuwa kamwe ndani ya mwaka huu wa 2012 hatakubali
kuona hali hiyo inajitokeza kama
ilivyojitokeza kwa mwaka 2011 na badala yake shule ambayo itajitokeza na hali
hiyo ni lazima ichukuliwe sheria kali kabisa.
“leo mpo hapa wamiliki na mameneja wa shule kama mnataka
kushika nafasi za kwanza hakikisheni kuwa mnawafundisha watoto wenu kwa bidii
na wala sio kuwapa majibu na shule yeyote itakayofanya hivyo mwaka huu nilazima
ifutiwe usajili kwa kuwa wanaopata shida ni hawa wanafunzi”alisema bw Mkombole.
Awali aliwataka wamiliki wa shule pamoja na Mameneja wa
shule binafsi kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kuajiri walimu wenye sifa
kwa kuwa walio ambao hawana sifa ndio chanzo pekee cha kuwapa watoto mbinu za
udanganyifu ili waonekane kama wamefanya vema
kumbe wamedanganya Jamuhuri.
Mkombole alisema kuwa ili shule iweze kushika nafasi za
kwanza zinatakiwa kuwa na walimu wenye ubora ambao unaitajika kwa kiwango cha
hali ya juu ambapo kwa kufanya hivyo pia wataimarisha hata uchumi wa nchi
Katika hatua nyingine
Mwenyekiti wa chama hicho cha wamiliki wa shule binafsi kwa mkoa wa Arusha
Ester Lema alisema kuwa pamoja na kuwa shule hizo zimekuwa ni msaada mkubwa
sana kwa mkoa wa Arusha lakini bado zinakabiliwa na changamoto kubwa sana .
Lema alitaja changamoto kubwa ambayo kwa sasa wanakabiliwa nayo ni pamoja
na changamoto ya ulipaji wa kodi kubwa sana
huku nao wakiwa wanachangia kusaidia Serikali kuhusiana na kuwaelimisha watoto
wa Kitanzania,
Aliitaka Serikali kuweza kuangalia tena mchakato wa kodi
kubwa sana hasa kwa shule binafsi kwa kuwa changamoto hiyo nayo imekuwa ni
mzigo mkubwa sana kwa wamiliki na hata Mameneja wa shule binafsi.
No comments:
Post a Comment