Saturday, April 20, 2013

WIKI YA CHANJO 22-28 APRIL 2013

Tanzania nimiongonni mwa nchi  ambazo tarehe 22-28 april 02013 zitaungana  na nchi nyingine duniani kote kuadhimisha wiki ya chanjo.

akifafanua kuhusu wiki ya chanjo kwa mwaka huu,kaimu katibu mkuu Bi ,Regina Kikuli wa Wizara ya afya na ustawi wa jamnii ameeleza kuwa maadhimisho ya  mwaka huu yatafanyika kitaifa  katika mkoa wa Pwani huku mikoa mingine yote nayo ikiadhimisha tukio hilo la wiki ya chanjo yatakayofanyika  nchi nzima kwa nagazi ya  mkoa ,wilaya  na vituo vyote vya kutoa hudama ya afya.

Umuhimu wa chanjo hii ni kuhakikisha kuwa  tunaokoa maisha ya  watoto kwa kuwapatia  huduma ya chanjo kwa watoto wote wenye umri wa chi ya mwaka  mmoja  ambao hawajapata chanjo au hawajakamilisha  ratiba ya  chanjo kama inavyostahili.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni ''OKOA MAISHA,JIKINGE NA  ULEMAVU ,PATA CHANJO''

Magonjwa mangine  yanayokingwa na  chanjo hapa nchini ni pamoja na DONDAKOO,KIFADURO,POLIO,SURUA,PEPOPUNDA,HOMA YA INI ,HOMA YA UTI WA MGONGO ,NIMONIA na KUHARA .

Maadhimisho haya yatafanyika  katika ngazi ya mkoa ,wilaya  na vituo vyote vya  kutoa huduma kwa jamii kwa kupitia  shughuli zifuatazo:


.Uhamasishaji  na uelimishaji jamii kwa ngazi ya mkoa wilaya  na vituo vya  vya kutolea huduma za afya kwa  shughuli zifuatazo.

. Kuelimisha  na kuhamasisha jamii  kuhusu  chanjo mpya  za kukinga NIMONIA na KUHARA ambazo zilianza kutolewa tangu january 2013.

.Zoezi  la chanjo litaanza kufanyika rasmi  kuanzia tarehe 22-28 mwezi april 2013  hivyo wananchi  wote wanaombwa  kutoa ushirikiano  katika  zoez zima  kwa kuwapeleka  watoto wote walio na umri chini ya mwaka mmoja  kupata chanjo hii haraka iwezekanavo ili kukamilisha zoezi hili kwa haraka.

aidha kaim katibu mkuu BI .REGINA KAKILU alimalizia kwa kuwakumbusha viongozi wote  na watendaji wa ngazi zote  kutoa ushirikiano  wa hali na mali  juu ya zoezi  hili ili kuhakikisha yafuatayo  yanafanyika kwa usahih:

1.Maadhimisho haya yanazinduliwa katika ngazi ya mikoa wilaya na vituo  vya kutolea huduma.

2.vituo vinafunguliwa kuanzia  saa mbili asaubuhi  hadi 11 jioni  ili kutoa fursa  kwa watoto kupata huduma ya  chanjo.

3.Kuwahamasisha wazi na walezi  wenye watoto kuwapeleka  watoto wao kupata chanjo  pia wakumbuke kwenda na vyeti vya watoto vya kliniki.

4kuwahamasisha wazazina walezi wa watoto ambao hawajapata chanjo wanapelekwa kwenye viyuo vya  chajo ili kupata chanjo.


No comments:

Post a Comment