Tuesday, June 5, 2012

Ferouz kutambulisha ‘Kibodaboda’ Dom

Masanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ferouz Mrisho 

Masanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ferouz Mrisho ‘Ferooz’ ameahidi kuwachezesha mtindo wake wa ‘Kibodaboda’ mashabiki watakaohudhuria onyesho la kumtambulisha Aslahi Isihaka ‘Dogo Aslay’ litakalofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.


Tamasha hilo ambalo litawashirikisha wasanii wengine mbalimbali,  linatarajiwa kufanyika Juni 9.

  Ferooz ambaye hivi sasa anatamba kwa nyimbo zake zilizopo kwenye albamu yake mpya ya ‘Rizevu’ zilizo kwenye mahadhi ya mchiriku, alisema mashabiki wa mjini Dodoma watapata bahati ya kuwa wa kwanza kuzisikia nyimbo zake mpya ambazo baadhi bado hazijasikika redioni.

“Ninawaambia wapenzi wangu na wapenzi wa bongo fleva kwa ujumla wasilikose onyesho la Dogo Aslay Live kwani nimewaandalia vitu ambavyo hawatavisahau, nitaimba nyimbo zangu zote mpya na nitawaonyesha jinsi ya kucheza Kibodaboda,” alisema Ferooz.


Msanii huyo aliyepata kutamba na wimbo wa ‘Starehe’ , hivi sasa anafanya vizuri pia na nyimbo za’Ndege Mtini’ aliomshirikisha Shoz Dia wa THT na ‘Tusitafutane’ aliomshirikisha 20 Pacent, ‘Sio Ize’ na ‘Rizevu’ uliobeba jina la albamu.


Naye Mratibu wa onyesho hilo Jacqueline Massano, alisema mbali ya Ferooz, wasanii wengine watakaotumbuiza ni pamoja na Mkubwa na Wanawe cha Temeke Sandali, kundi la TMK Wanaume Family, Mfalme wa Rhymes nchini Selemani Msindi ‘Afande Sele’ na mshindi wa tuzo tano za muziki za Kilimanjaro mwaka uliopita, 20 Parcent.

No comments:

Post a Comment