Tuesday, June 5, 2012

Epiq Bongo Star Search kuanzia Dom

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Production, Ritha Paulsen
 
Ziara ya kusaka vijana watakaoshiriki katika shindano la Epiq Bongo Star Search mwaka huu itaanzia mkoani Dodoma Juni 15 kwenye ukumbi wa Royal Village.

Akizungumzia ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark  Production, Ritha Paulsen, alisema kuwa washiriki wanatakiwa kufika kwenye ukumbi huo kuanzia saa 12:00 asubuhi.


Alisema kuwa kampuni yake inatarajia kuchukua vijana watatu hadi watano watakaouwakilisha mkoa huo katika kinyang’anyiro ambacho fainali zake zitafanyikia Dar es salaam.


Alisema kwamba wakiwa mkoani humo, wanatarajia kuona vipaji vya wasanii wa kila aina kwa kuwa EBSS inalenga kukuza vipaji vya vijana wenye uwezo wa kuimba aina zote za nyimbo.


“Kama ambavyo imeshafahamika kuwa mwaka huu, mshindi wa EBSS atapata kitita cha shilingi milioni 50 taslim…hivyo ni kwamba tunawaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma wenye vipaji kuja kwa wingi siku hiyo,” alisema Ritha


Ritha ataongozana na majaji wengine ambao ni Salama Jabir na Master Jay.  EBSS ya mwaka huu imedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel.

No comments:

Post a Comment