“PRESS RELEASE” TAREHE 24. 06. 2013.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA MOTO
MNAMO TAREHE 23.06.2013 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO ENEO LA DDC-MBALIZI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. TERESIA D/O MWAIJIBE, MIAKA 40, KYUSA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA MLIMA- RELI MBALIZI ALIGUNDUA KUUNGUA KWA VYUMBA KUMI [10] KATI YA VYUMBA KUMI NA MBILI [12] VYA NYUMBA YAKE NA KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI.
NYUMBA HIYO IMEPANGWA NA WAPANGAJI FAMILIA NNE [4] MOTO HUO ULIANZIA KATIKA CHUMBA CHA MPANGAJI KATABALO S/O RWEYEMAMU, MIAKA 32,MHAYA,FUNDI KUCHOMELEA MKAZI WA DDC – MBALIZI .
CHANZO CHA MOTO HUO AMBAO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI JIJINI MBEYA, JESHI LA POLISI NA WANANCHI BADO KINACHUNGUZWA.
THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA NA HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA.KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA NA TAHADHARI NA MAJANGA YA MOTO ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA GARI KUGONGA GARI NA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO
MNAMO TAREHE 23.06.2013 MAJIRA KATI YA SAA 23-00HRS NA SAA 00:30HRS HUKO ENEO LA FOREST KARIBU NA BENKI KUU BARABARA YA MAHAKAMA KUU JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIGONGA GARI T.741 BXU AINA YA MARCH LILILOKUWA LIMEEGESHWA ENEO HILO KISHA KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASKARI POLISI AITWAYEEX.G.9386 PC PATRICK,MIAKA 23,MGOGO WA KIKOSI CHA FFU- MBEYA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO . CHANZO KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMESAFIRISHWA KWENDA DODOMA KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO DEREVA NA GARI LILILOHUSIKA NA AJALI HII AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment