Sunday, March 9, 2014

Muungano wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotetea haki za Wanawake yasherehekea Siku ya Wanawake Duniani

Kutoka kushoto ni Miss Tanzania 2013 Happy Watimanywa , Dk. Agnes Nyomola kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye ni Mtaalam wa mambo ya Sayansi, na Specioza Rweyemamu ambaye ni Ispecta katika mambo ya anga katika Mamlaka wa usafiri wa Anga Tanzania, ambao ndio walikuwa wasemaji katika sherehe hizo
Specioza Rweyemamu ambaye ni Ispecta katika mambo ya anga katika Mamlaka wa usafiri wa Anga Tanzania akizungumza na wanafunzi pamoja na wageni waalikwa mbalimbali hasa wanafunzi na kuwaasa kuwa wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii na kusoma kwa bidii kwani hakuna kisicho wezekana kila mtu anaweza, pia amewasihi wasichana hasa wadogo kupenda kusoma zaidi ili waje kuwa viongozi wa baadaye.
Wakili wa Mahakama Kuu Modesta Mahiga akizungumza na wanafunzi waliofika katika Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Chuo Kikuu Dar es salaam na kuwahimiza wanafunzi hasa wakike wanaokuwa wasikimbilie katika mambo makubwa lakini wakazane na masomo ili kupata kufanikiwa zaidi.
Miss Tanzania 2013 Happy Watimanywa akiongea na wanafunzi, alisisitiza sana wanafunzi wenzake wa kike kuwa wanatakiwa kusoma kwa Bidii ili kuweza kuja kufanikiwa katika mambo yao ya mbeleni, aliongeza kuwa mtoto wa kike ndio taifa la kesho na kiongozi wa kesho hivyo  ni lazima wakazane sana katika masomo yao na kuichukulia siku ya leo kama changamoto na chachu kwao ya kujibidisha zaidi.
Mwenyekiti wa Muunganiko wa mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotetea haki za Wanawake Tanzania Bi. Juliana Bwire akitoa neno la Shukurani kwa wasemaji wote waliokuwa wakizungumza kila mmoja kwa wakati wake , pia kuwashukuru wote waliofika katika Sikukuu hiyo ya Mwanamke Duniani.
Jane Mrema, Mshauri wa Jinsia  kutoka Shirika la Plan International akielezea nia yao kubwa ya kushiriki katika Sherehe hizo leo.
Gloria Chambo, mwanachama  wa chama cha Muunganiko wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ambaye ndiye alikuwa mshereheshaji wa Siku hiyo ya wanawake akizungumza Jambo wakati wa Sherehe hizo na kuongoza ratiba hiyo.


Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali kutoka Jijini Dar es Salaam wakiwa wanafuatilia mambo mbalimbali yanayo endelea wakati wa sherehe hizo.
Hawa ni wanafunzi wa Chuo cha Ufundi kwa watu wenye ulemavu walemavu wa jumla, wakiwa wanafuatilia kwa umakini kinacho endelea uwanjani hapo.
Msichana mfupi, mbele ni Mwanafunzi wa  Chuo cha Ufundi kwa watu wenye ulemavu, Jovina Vedastus  ambaye ni Fundi wa Ushonaji na utengenezaji wa Batiki akicheza muziki ambapo alikonga nyoyo za watu wengi kwa umahili wake huo katika kucheza.
 Wasemaji wakifurahia Burudani mbalimbali zinazo endelea.
 wanafunzi wa Chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu walemavu wa jumla, hapa wakiwa viziwi, wasio ona, wenye ulemavu wa Miguu , mikono mapoja na Matatizo mengine wakiwa wanatumbuiza na burudani ya aina yake ambapo watu wengi walivutiwa sana na kufurahishwa.
 Banana Zoro akitoa Burudani ya uhakika pamoja na Bendi yake wakati wa maadhimisho hayo.
Mwakilishi kutoka OXFAM ambao pia ni wanachama wa  chama cha Muunganiko wa mashirika yasiyo ya Kiserikali  Afisa utetezi wa haki  za kiuchumi OXFAM Bi.Mkamiti Mgawe  akifunga Rasmi sherehe hizo na kuwashukuru wote waliofika katika katika sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es salaam leo.
Hili lilikuwa ni Tukio la Aina yake ambapo Miss Tanzania 2013 Happy Watimanywa alipo vamiwa na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Sekondari Jijini Dar es salaam wakiomba awasainie katika Madaftari yao kama kumbukumbu ya kwamba na wao walisha wahi kumuona Mrembo huyo, Hapa akiwa anasaini katika Baadhi ya Madaftari hayo.

No comments:

Post a Comment