|
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Prof. Idris Alli Mtulia akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Kituo hicho.
|
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa nchini (MSD) akitoa taarifa fupi ya MSD kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo kipya.
|
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii Dk Stephen Kebwe Aliyemwakirisha Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamerd Ghalib Bilal akihutubia
viongozi, watumishi wa MSD na wananchi wakati wa uzinduzi wa kituo
kipya cha MSD Wilayani Muleba
|
Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini
Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi akitoa hotuba ya shukurani za wananchi wa Wilaya ya
Muleba na Mkoa wa Kagera kwa kuzinduliwa kwa kituo kipya cha MSD
Wilayani Muleba.
|
Baadhi ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali ya uzinduzi wa kituo kipya cha MSD Muleba.
|
Baadhi ya wanawake wakifuatilia tukio la uzinduzi .
|
Kazi ni moja tu kushambulia ndani ya viwanja vya uzinduzi wanamuziki wa Kakao Bandi.
|
Ramani kuonyesha Mfumo wa Usambazaji
Dawa kutoka MSD kwa kauli mbiu yake kufikisha dawa moja kwa moja hadi
vituo vya kutolea huduma za afya ikiwa ni Zahanati, Vituo vya Afya,
Hospitali za Wilaya na Teule, Mkoa na Rufaa maeneo yote nchini.
|
Baada ya kumalizikehe kwa sherehe za
uzinduzi Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini alianzisha maandamano ya Amani
kuunga mkono juhudi za serikali kufikisha huduma ya dawa na vifaa tiba
kupitia Bohari Kuu ya Madawa (MSD) nchini kote ili kupunguzi vifo vya
mama na watoto, mapambanaona ugonjwa wa UKIMWI na Malaria.
|
Na Peter Fabian.
ALIYEKUWA MULEBA.
MAKAMU wa
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal
ameiagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kushirikiana na Jeshi la
Polisi nchini kufanya msako endelevu ili kuwafichua, kuwakamata na
kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaopatikana na Dawa za
Serikali kinyume cha taratibu na sheria zilizopo.
Katika
hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii Dk. Stephen Kebwe (MB) wakati wa ufunguzi rasmi wa
Kituo cha Kutunza na Usambazaji Dawa (Bohari ya MSD) cha muda kilichopo
eneo la Mahalahala kwenye Hospitali inayojengwa ya Wilayani Muleba juzi
alisema wizi na upotevu wa dawa hizo zinazotolewa na serikali hufanywa
na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.
Alieleza
kwamba Kituo cha Muleba (Bohari ya Madawa ya MSD) cha muda kitakuwa na
jukumu kubwa la kusambza dawa na vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali na
Vituo vya Afya katika maeneo yote ya Wilaya za Mikoa ya Kagera (Vituo
270 ) na Geita (Vituo 64) kuanzia mwezi julai mwaka 2013 mfumo huu wa
usambazaji dawa ulianza kabla ya kufunguliwa rasmi.
Makamu
wa Rais Dk. Katika hotuba hiyo ameipongeza Bohari Kuu ya Madawa (MSD)
nchini kwa kuanzisha utaratibu wa kuweka alama ya Government Of Tanzania
(GOT) katika dawa zinazosambazwa na kusema kuwa hatua hiyo itasaidia
dawa za serikali kutambulika kiurahisi kwa wananchi pamoja na kuthibiti
wauzaji wa maduka ya dawa baridi wanaopelekewa zinazoibiwa na watumishi
wa serikali.
“Lengo
kubwa la kufunguliwa kituo hichi ni kupunguza vifo vya akina mama na
watoto, kupambana na ungonjwa wa UKIMWI na Malaria ikiwa ni kuanza
kutumia mfumo wa fikisha dawa karibu na wananchi na kwa wakati ili
kufanikisha lengo mahususi la serikali ya awamu ya nne huku ufatiliaji
wake uwe chini ya usimamizi wa karibu na matumizi ya dawa zinazosambazwa
kwenye vituo vya huduma ” alisisitza
Kwa
upande wake Naibu Waziri Dk. Kebwe amesikitishwa na taarifa ya kasi ya
wizi na upotevu wa dawa zinazopelekwa na serikali kupitia Bohari ya Dawa
(MSD) katika Wilaya za Ngara, Kerwa, Biharamulo na Muleba huku
akizipongeza Wilaya za Karagwe na Bukoba vijijini kwa kuweka jukumu la
udhibiti wizi na upotevo wa dawa hizo kutoka kwa watumishi wasio
waadilifu.
Dk. Kebwe ameungana na
Makamu wa Rais Dk. Bilal kuzitaka Kamati za ulinzi na usalama za Mikoa
ya Kagera na Geita na zile za Wilaya kwa kushirikiana na Wakurugenzi na
Wenyeviti wa Halmashauri zote kufatilia kwa ukaribu huku akitaka taarifa
za upokeaji dawa na utolewaji kwa wananchi utolewe kwenye Vikao vya
Kamati ya Ushauri na Maendeleo (RCC) za Mikoa yote.
“Tusikubaliane na
wajanja wachache wa Idara za Afya kutumia mwanya wa kuiba dawa na
kuziuza kwenye maduka waliyoanzisha na kisha kujinufaisha kwa kununua
magari, kujenga vyumba za kifahari nasi kuwashangilia eti muda mchache
jamaa ana gari zuri ambapo makusanyo ya mapato kutoka vituo vya afya
kuonyesha ni asilimia 50 tu huku zingine zikiliwa na wajanja wachache”
alisema.
Dk.
Kabwe alisema kuwa Wizara yake itatumia bilioni 6 kwa mwaka katika Dawa
zote zitakazotolewa na kituo hicho na kila mwezi kitasambaza dawa za
kiasi cha shilingi milioni 150 huku Bajeti ya Wizara ikionekana kutumia
Bilioni 80 za Dawa, Vifaa tiba na Vitenganifu na kupitia kituo hicho
ndani ya siku 14 Hospitali na Vituo vya Afya vitapeka oda na kupatiwa
dawa.
Awali Mwenyekiti wa
Bodi ya Wadhamini wa MSD, Porfesa Idrisa Mtulia kuzinduliwa kwa kituo
hicho ni mkombozi mkubwa wa wananchi wa Mkoa ya Kagera na Mkoa wa jirani
wa Geita na Wilaya zake zote ambapo kitawezesha upatikanaji wa dawa,
vifaa tiba na viunganifu vya kutolea huduma ya afya kwa Bohari ya madawa
kufikisha haraka huduma zake kwa wateja.
Prof.
Mtulia alisema kwamba pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili MSD
itahakikisha inashirikiana na serikali na wadau wengine kuendelea kutoa
huduma bora na kufikisha dawa zenye ubora na bei nafuu wakati wote kwa
manufaa ya watanzania wote huku akihimiza Halmashauri zote nchini
kukunua dawa kutoka MSD kwa kutumia vyanzo vyake vingine vya fedha.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) nchini
Cosmas Mwaifwani alisema kwamba kutokana na ukubwa wa Kanda ya Ziwa na
idadi kubwa ya wingi wa watu zaidi ya milioni 13 kutokana na matokeo ya
Sensa ya mwaka 2012 kuwepo na malalamiko ya wadau mbalimbali juu ya
huduma za MSD Kanda ya Mwanza kutokidhi kwa wakati huduma ya utoaji wa
dawa.
Kaimu
huyo alieleza kuwa imefungua kituo hicho cha muda kuhakikisha
upatikanaji na usambazaji wa Kituo cha Muleba kinafanikisha lengo la MSD
na kupunguza usumbufu wa Mkoa wa Kagera kufata huduma hiyo Jijini
Mwanza na Kanda ya Tabora ambapo ilionekana kuchelewesha upatikanaji wa
dawa, vifaa tiba vyenye ubora na kwa bei nafuu kwa watanzania wote.
“Ufunguzi
wa Kituo hiki cha usambazaji dawa Mkoani Kagera na Mkoa wa jirani wa
Geita ni mchango mkubwa wa utekelezwaji wa Malengo ya Millenia hususani
kupunguza vifo vya mama na watoto na kupambana na Ukimwi na Malaria
ambayo imekuwa ni magonjwa ya mlipuko katika maeneo mengi ya Wilaya za
Muleba ” Alisema Mwaifwani.
Mbunge
wa Muleba Kusini Porfesa Anna Tibaijuka ambaye ni Waziri wa Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwahakishia Naibu Waziri Dk.
Kebwe na uongozi wa MSD kuwa eneo la Ekhali 5 zilizotolewa na
Halmashauri Wilaya ya Muleba linaachwa wazi ili kutoa nafasi kwa MSD
kujenga Ofisi kuu na Maghala ya kuhifadhiwa dawa Mkoani humo.
“Kituo
hiki ni wajibu wetu kukilinda na kukitunza vizuri ili kiendelee kutoa
huduma, lakini Mkurugenzi wa Halmashauri naomba utumia sheria za ardhi
zilizopo kuhakikisha unawaondosha watu wanaovamia eneo tulilotenga kwa
ajili ya shughuli za MSD hili ni agizo natoa kama Waziri nila serikali
siyo langu kama Mbunge wa Jimbo hili” alisisitiza.
Mbunge
huyo aliongeza kuwa kutokana na waathilika wakubwa ni Kimama na watoto
pamoja na Wilaya hiyo kukubwa na magojwa ya mlipuko hususani Malaria
ambayo yalipelekea serikali na Wizara ya Afya kutuma wataalamu na
kufanya utafiti kisha kuanzisha mkakati wa kupulizia dawa ya Ukoko
kwenye nyumba za Wilayah ii ili kudhibiti ugonjwa huo uliokuwa ni janga
kwa wananchi.
HABARI KWA HISANI YA MICHUZI BLOG
No comments:
Post a Comment