Tuesday, June 5, 2012

Mgogoro wafugaji, wakulima wafukuta

Mgogoro baina ya wakulima na wafugaji wa vijiji vya Kata ya Makuyuni umezidi kufukuta baada ya baadhi ya vigogo wa serikali ya wilaya hiyo kudaiwa kuuendeleza kwa manufaa binafsi.

Madai hayo yalitolewa jana na wakazi wa Kijiji cha Gombaram kilichopo kata hiyo .


Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Laulent Doviko alidai kuwa mgogoro huo ulianza tangu mwaka 2006 na kwamba hadi sasa haujapatiwa ufumbuzi licha ya mwaka 2007 kusababisha mapigano baina yao na wafugaji na kujeruhiwa watu kadhaa akiwamo yeye.


 Alidai kuwa  chanzo cha mgogoro huo ni wafugaji kutoka Kata jirani ya Bungu kupitisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima Mtendaji wa Kijiji cha Gombaran, Adam Bakari alithibitisha kuwapo kwa  mgogoro huo na kesi mahakamani.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe, Laulent Shauri alithibitisha   kupata taarifa za mgogoro huo na kesi hizo mahakamani lakini alikanusha kujihusisha nao kama inavyodaiwa na wanakijiji hao.


 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment