Thursday, June 14, 2012

Mauwaji yashamiri Baghdad

Mashambulio dhidi ya mahujaji wa madhehebu ya shia nchini Iraq yazidi kuuwa watu, huku taarifa zaidi zikisema kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka.
Wanamgambo wenye msimamo mkali wa kiislamu na wenye mafungam na mtandao wa al-Qaeda. Kiasi ya mahujaji 56 wameuawa hii leo nchini Iraq kufuatiwa na mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa mjini Baghdad.

Mashambulio hao pia yanawalenga polisi ambapo watano tayari wameuawa wakiwa kwenye vituo vya ukaguzi baada ya watu waliokuwa na silaha kuwafyatulia risasi kusini mwa mji huo.
Idadi hiyo ya vifo huenda ikaongezeka kutokana na kushamiri kwa mashambulio ya mabomu yanayotegwa kwenye magari. Misikiti minne kwenye maeneo mbalimbali ya Baghadad imeshambuliwa wakati mahujaji hao wakiwa kwenye ibada hii leo.
Mashambulio hayo ni ya tatu kufanywa kwenye mji huo katika kipindi cha wiki moja dhidi ya watu hao walioko kwenye ibada ya kumbukumbuku ya imamu wao, Moussa al-Kadhim.
Kitisho cha al-Qaeda
Ghasia zimepungua nchini Iraq tangu kumalizika kwa uvamizi wa Marekani nchini humo, lakini sasa wanamgambo wwa kiislamu wenye msimamo mkali wanofungamana na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda bado ni tishio.

 Mji wa Baghdad Mji wa Baghdad
Lengo ni kuufufua mzozo wa madhehebu uliokuwepo hapo kabla ambao ulitaka kuiingiza nchi hiyo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe katika kipindi cha mwaka 2006 hadi 2007.
Vituo vya ukaguzi vimeongezwa wiki hii baada ya maelfu ya mahujai kuwasili mjini Baghadad kuutembelea msikiti wa uliopo kwenye wilaya ya Khadhimiyah kaskazini mwa mji huo ambako ndiko hufanyika kumbukumbu hizo.
Waziri Mkuu Nur al- Maliki asema hizo ni hujuma kwake
Waziri Mkuu wa Iraq anayetokea madhehbu ya shia, Nur al- Maliki, anasema mashambulio hayo yamefanywa na watu wa madhehebu ya Sunni, Wakurdi na wapinzani wengine wa madhehebu yake ya Shia ili baade wampigie kura ya kutokuwa na imani naye.

Moja ya mashambulizi mjini Baghdad Moja ya mashambulizi mjini Baghdad
Wapinzani wanamlaumu al-Maliki kwa kuimarisha nguvu zake na kushindwa kutimiza ahadi ya kugawana madaraka baina ya pande zote.
Mapema mwezi huu, watu 26 waliuawa na wengine 190 walijeruhiwa baada ya bomu lililotegwa kwenye gari kuripuka mbele ya ofisi ya madhehebu ya shia mjini Baghdad. Wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo mkali walisema wanahusika na mashambulizi hayo.
Hofu imetanda miongoni mwa raia wa nchi hiyo, wakihisi huenda mashambulizi hayo yakafungua mlango kwa machafuko yanayotokana na mzozo wa madhehebu kama yale ya mwaka 2006-2007.
Mwaka uliopita, mahujaji ya madhehebu ya shia walifanya ibada zao bila kutokea kwa matukio ya aina hiyo, na kuvifanya vikosi vya usalama vya nchi hiyo kujihisi vimefanya kazi yao ya ulinzi ipasavyo.

No comments:

Post a Comment