Waandamanaji Misri
Hali ya hatari ambayo imekuwa
ikitumika nchini Misri kwa miongo mitatu na kuyapa majeshi ya usalama ya
Misri madaraka ya kupindukia kwa kuwakamata washukiwa na kuwafikisha
katika mahakama maalum, imeondolewa.
Watawala wa kijeshi wa Misri ambao walitwaa madaraka baada ya Rais Hosni Mubarak kung'olewa madarakani mwaka jana walionyesha kuwa wasingeirejesha tena sheria hiyo baada ya kumalizika muda wake usiku wa kuamkia leo.
Kuondolewa kwa sheria hiyo, lilikuwa dai kubwa la waandamanaji wapenda demokrasia ambao walichochea uasi dhidi ya Bwana Mubarak.
No comments:
Post a Comment