TEKNOLOJIA
ya kutumia simu kufukuza mbu nyakati za usiku imeingia
nchini.Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Gerald Simbo
aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwamba simu yake ina
uwezo wa kufukuza mbu usiku inapowekwa kwa kutumia mfumo wa 'Mosquito
repellant'.
Simbo alisema simu yake inayojulikana kwa jina la
"Samsung Galaxy Pocket ina uwezo wa kufukuza mbu kama itawekwa kitandani
wakati wa kulala.
Alisema simu hiyo aliinunua kwenye kampuni
SamSung Tanzania. Meneja wa Samsung Tanzania, Kishor Kumar alipoulizwa
jana kuhusiana na kauli hiyo alikiri kuwa na aina hizo za simu na kwamba
sasa zinasambazwa nchini na kuuzwa kwa gharama ya Sh200,000.
"Kwa
ujumla simu hii ni ya kisasa inayokidhi mahitaji ya mawasiliano kwa
Watanzania na zaidi inakuja na ofa nyingine ikiwemo kadi ya simu na
Airtel bundle, pia ina mfumo ambao endapo itaibiwa mmiliki na uwezo wa
kuifunga ,"alisema Kumar.
Naye mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam, Enock Kweka alisema anaitumia simu ya aina hiyo kufukuza mbu
nyumbani kwake na kuhifadhi nyaraka muhimu anazotumia katika masomo
yake.Ilielezwa kwamba ina mtandano wa kompyuta wa 250 MB kwa muda wa
mwaka mmoja.
|
|
No comments:
Post a Comment