Sunday, February 9, 2014

YANGA ILIVYOICHAPA COMORO MABAO 7 KWA NUNGE KATIKA UWANJA WA TAIFA


 Timu zikiingia uwanjani kwa ajili ya mpambano wao wa kwanza wa mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika, Uwanja wa Taifam Dar es Salaam jana jioni. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wachezaji wa Yanga ya Tanzania na Komorozine ya Comoro, wakiingia Uwanja wa Taifa, tayari kwa mchezo huo leo.
Wachezaji wa Yanga ya Tanzania na Komorozine ya Comoro, wakiingia uwanjani.
 Kikosi cha Yanga Africa kikipiga picha kabla ya mchezo huo.
Kikosi cha timu ya Komorozine cha Comoro kikipiga picha kabla ya mchezo huo.
 Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo huo.
Haruna Niyonzima wa Yanga ya Tanzania (kushoto), akitafuta mbinu ya kumtoka Mohamed Erefeda wa Komorozine ya Comoro.
Haruna Niyonzima wa Yanga ya Tanzania akiwania mpira uliokuwa ukidhibitiwa na MoidjieAli wa Komorozine ya Comoro.
Wachezaji wa Yanga na Komorozine wakibadilishana mabenchi ya kukalia kutokana na kila timu kukaa katika benchi ambalo si la kwake kwa mujibu wa mchezo wa kuwa mwenyeji wa mchezo.
Wachezaji wa akiba na makocha wa Yanga, wakondoka kwenye benchi walilokaa na kuwapisha Komorozine ya Comoro.
 Simon Msuva wa Yanga, akikimbia na mpira huku akifuatwa na Ahamadi Houmad wa Komorozine.

Beki wa Komorozine Spots ya Comoro, Ahamadi Houmad, akilala chini kuondoa hatari, wakati kiungo wa Yanga, Haruna Niyozima alipokuwa akijaribu kumtoka kuelekea kwenye lango la timu hiyo, wakati wa mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika, ulichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga ilishinda mabao 7-0.
Ngassa akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Mohamed Erfeda wa Komorozine Sports
Ngassa wa Yanga na Mohamed Erfeda wa Komorozine Sports wakipambana
Mouayade Almansoor wa Komorozine, akipambana na Simon Msuva wa Yanga.
 Moidjie Ali wa Komorozine akipiga mpira kichwa.
Hamisi Kiiza wa Yanga (20), akiruka kuupiga kichwa mpira sambamba na Ahamadi Houmadi (2) wa Komorozine ya Comoro.
 Beki wa Komorozine Spots ya Comoro, Ahamadi Houmad, akilala chini kuondoa hatari, wakati kiungo wa Yanga, Simon Msuva alipokuwa akijaribu kumtoka kuelekea kwenye lango la timu hiyo, wakati wa mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika, ulichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga ilishinda mabao 7-0.

 Nadir Haroub 'Canavaro' akiruka juu kuupiga kichwa mpira.
Ali Mohamed wa Komorozine, akiwania mpira na Simon Msuva wa Yanga.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo, lililofungwa na Mrisho Ngassa (katikati), dhidi ya Komorozine Spots ya Comoro, wakati wa mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika, ulichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga ilishinda mabao 7-0.
Wachezaji wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', (katikati), Hamis Kiiza aliyebebwa na Simon Msuva, wakishangilia bao la pili la timu hiyo, lililofungwa na Canavaro dhidi ya timu ya Komorozine Spots ya Comoro, wakati wa mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika, ulichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga ilishinda mabao 7-0.
Simon Msuva wa Yanga, akikimbia na mpira kuelekea kwenye lango la Komorizine.
Abdou Moussoidi wa Komorozine, akimkwatua Simon Msuva wa Yanga.
Mourtadhoi Fayssoil wa Komorozine akiudhibiti mpira uliokuwa ukiwaniwa na Simon Msuva wa Yanga.
Mourtadhoi Fayssoil wa Komorozine akiwania mpira na Simon Msuva wa Yanga.
Mourtadhoi Fayssoil wa Komorozine akiwania mpira na Simon Msuva wa Yanga.
Mrisho Ngassa wa Yanga, akiudhibiti mpira mbele ya Ali Mohamed wa Komorozine ya Comoro.
Haruna Niyonzima wa Yanga, akiwania kumtoka Ali Mohamed wa Komorozine ya Comoro.
Haruna Niyonzima wa Yanga, akimpiga chenga Moidjie Ali wa Komorozine ya Comoro.
Simon Msuva wa Yanga, akiwania mpira na Imroina Ismael wa Komorozine.
Simon Msuva wa Yanga, akimtoka Imroina Ismael wa Komorozine.
Golikipa wa Komorozine, Attoumani Farid, akiwa kapotea kabisa huku mabeki wake nao wakiwa wamechanganyikiwa baada ya Hamisi Kiiza (kushoto) na Haruna Niyonzima kugongeana mpira kwenye eneo la timu hiyo ya Comoro.
 Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao katika mchezo huo.
Golika wa Komorozine, Attoumani Farid, akiwa ameshapitwa na mpira uliopigwa na Didier Kavumbagu na kuandika bao la 6 kwa timu ya Yanga ya Tanzania. 

Hadi wakati huo, Yanga ilikuwa ikiongoza kwa mabao 6-0.
 Yanga wakifunga bao la 7 katika mchezo huo.
Beki wa Komorozine, Ahamadi Houmad (kushoto), akiwania mpira na Haruna Niyozima wa Yanga katika mchezo huo.
Beki wa Komorozine, Ahamadi Houmad (kushoto), akiwania mpira na Haruna Niyozima wa Yanga.
 Hadi mwisho wa mchezo huo, ubao wa matangazo ulikuwa ukisomeka Yanga FC 7, Komorozine Sport 0.
 Mbuyu Twite wa Yanga, akimdadisi jambo kampeni wa timu ya Komorozine, Mohamed Erefeda 
Kampeni wa timu ya Komorozine, Mohamed Erefeda, akimweleza jambo Mbuyu Twite wa Yanga, mwisho wa mchezo huo.
Mrisho Ngassa (kulia), akiwa na mpira wake aliokabidhiwa baada ya kuifungia timu yake ya Yanga mabao 3 katika mchezo huo, timu yake iliyoibuka na mabao 7-0. Anayempongeza na Nahodha wake, Nadir Haroub 'Canavaro'.
Mrisho Ngassa (kulia), akipongezwa na Nahodha wake, Nadir Haroub 'Canavaro', baada ya kukabidhiwa mpira wake.

No comments:

Post a Comment