Sunday, February 9, 2014

NAPE ASEMA :KUWAZUIA WATU KUPIGA KURA NI KUHUJUMA DEMOKRASIA

 Katibu wa NEC tikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Nyasura wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani ambapo aliwaeleza wananchi haikuwa rahisi kuwaleta watanzania pamoja,hivyo basi wakatae kabisa vyama viinavyotaka kuwatenganisha kwa misingi ya udini na ukabila.
 Wakazi wa kata ya Nyasura wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani zinazoendelea nchi nzima ambapo kata 27 zitafany uchaguzi wa madiwani.
 Wakazi wa Kata ya Nyasura wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Nape Nnauye ambaye aliwaambia safari hii CCM haipo tayari kuhujumiwa na kutaka watu wengi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura na kutoa wito kwa vijana kulinda wapiga kura wa CCM.
Mgombea wa Udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Nyasura  Ndugu Alexander Mwikwabe akiomba kura toka kwa wananchi wa Nyasura kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Nyasura ambapo mgeni wa heshima alikuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Februari 7,2014.

No comments:

Post a Comment