Sunday, June 24, 2012

'Tanesco haitaongeza gharama'

Afisa Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud
 
Shirika la Umeme nchini (Tanesco), limesema licha ya kusema litaongeza gharama kwa watumiaji wa umeme mwezi ujao, lakini kwa sasa halina mpango huo.


  Afisa Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud amesema kwa sasa shirika halijakaa na kuamua iwapo gharama za umeme zipande ama la, licha ya awali kutaka zipande.

“Kwa sasa shirika halijaamua lolote, kwa sababu hatuna mpando huo hadi hapo itakapoamuliwa kivingine,” alisema Masoud.

Masoud amesema hayo baada ya waandishi  kutaka kujua iwapo nia yao ya kuomba kuongeza gharama za malipo ya umeme kwa mteja bado lpo mwezi ujao, licha ya bajeti ya serikali iliyotangazwa na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa hivi karibuni kupunguza gharama za mafuta ya kuendeshea mitambo mbalimbali.

Kutokana na hilo, msemaji huyo wa Tanesco alisema shirika lake halijapanga kukutana kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo, hivyo gharama zilizopo sasa zitaendelea kutumika hizo hizo.

No comments:

Post a Comment