Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inakamilisha maandalizi ya kufanya
Sensa ya Watu na Makazi ambayo itafanyika tarehe 26 Agosti, 2012. Ili
kufanikisha Sensa hii, Serikali inatangaza nafasi za kazi za muda za
MAKARANI NA MAKARANI WAANDAMIZI WA SENSA kwa Watanzania wenye nia na
sifa zinazostahili kama ilivyoainishwa katika tangazo hili. Kazi hii
itaanza tarehe 06 Agosti, 2012 na kumalizika tarehe 14 Septemba 2012.
1. KARANI WA SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji
wa nafasi hii, endapo atachaguliwa atapangwa katika eneo analofanyia
kazi au eneo analoishi na atakuwa na kazi zifuatazo:-
a) Kuhudhuria mafunzo ya kuhesabu watu;
b)
Kuhesabu watu kwa kutumia dodoso fupi katika Eneo la Kuhesabia Watu na
kuhakikisha kuwa kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu;
c) Kutunza vifaa vyote na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama; na
d) Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake.
Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a) Awe na umri usiozidi miaka 60 na mwenye afya njema;
b) Awe amehitimu angalau kidato cha nne;
c)
Awe ni Mkaguzi au Mratibu wa Elimu, Mwalimu katika Chuo cha Ualimu,
Shule ya Sekondari au Shule ya Msingi (Shule za Serikali au Binafsi)
katika eneo husika, AU
d) Awe ni mfanyakazi yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika, AU
e) Kijana aliyehitimu masomo yake na hajapata ajira, na
f) Asiwe na kesi yoyote ya jinai.
2. KARANI MWANDAMIZI WA SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji
wa nafasi hii, endapo atachaguliwa atapangwa katika eneo analofanyia
kazi au eneo analoishi na atakuwa na kazi zifuatazo:- 2
a) Kuhudhuria mafunzo ya kuhesabu watu,
b)
Kuhesabu watu kwa kutumia dodoso refu katika Eneo la Kuhesabia Watu na
kuhakikisha kuwa kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu,
c) Kutunza vifaa vyote na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama, na
d) Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake.
Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a) Awe na umri usiozidi miaka 60 na mwenye afya njema,
b) Awe amehitimu angalau kidato cha sita,
c)
Awe ni Mkaguzi au Mratibu wa Elimu, Mwalimu katika Chuo cha Ualimu,
Shule ya Sekondari au Shule ya Msingi (Shule za Serikali au Binafsi)
katika eneo husika, AU
d) Awe ni mfanyakazi yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika, AU
e) Kijana aliyehitimu masomo yake na hajapata ajira, na
f) Asiwe na kesi yoyote ya jinai.
3. Namna ya Kutuma Maombi
Mtanzania
mwenye sifa zilizotajwa hapo juu atume maombi yake kwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Sensa ya Wilaya/Halmashauri kwa anuani iliyowekwa hapa chini,
akiambatisha nakala za vyeti na nyaraka muhimu ili kuonyesha sifa
alizonazo.
Maombi
hayo yatumwe kwa kujaza Fomu Maalum ya maombi ya kazi ambayo
inapatikana katika Ofisi ya Mratibu wa Sensa wa Wilaya/Halmashauri, na
endapo fomu haikupatikana, mwombaji atume maombi kwa kuandika barua
akionyesha anuani kamili ya mahali anapofanyia kazi na namba ya simu
kama anayo.
Maombi
yapitishwe kwa wakuu wa kazi kwa walioajiriwa au Watendaji wa
Mtaa/Kijiji kwa wale wasiokuwa na ajira, ili maombi hayo yafike wilayani
kabla ya tarehe 25 Julai, 2012.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Wilaya
Wilaya ya ………………………..
S.L.P……………………………….……
Bofya maandishi yafuatayo kupakua:
No comments:
Post a Comment