Friday, June 29, 2012

Karadzic aondolewa moja kati ya mashitaka mawili

Mahakama ya uhalifu wa kivita kuhusu Yugoslavia imemwondolea kiongozi wa Waserbia wa Bosnia Radovan Karadzic moja kati ya mashitaka mawili ya mauaji ya kimbari, yanayomkabili.
 Uamuzi huo umetolewa jana ikiwa ni awamu ya katikati ya kesi dhidi yake iliyoendelea kwa muda mrefu.

Hatua ya kumwondolea moja kati ya mashitaka yanayomkabili ni pigo kwa waendesha mashitaka, lakini majaji wameyabakisha mashitaka mengine 10, ikiwa ni pamoja na kosa la mauaji ya halaiki ya Waislamu 8,000 katika eneo la Srebrenica mnamo mwaka 1995.

 Majaji walisema waendesha mashitaka hawakuwasilisha ushahidi wa kutosha kuthibitisha kosa hilo la mauaji ya kimbari linalohusisha mauaji ya kikatili, kufukuzwa na kuteswa kwa waislamu na WaCroatia katika miji ya Bosnia kulikofanywa na wanajeshi wa Serbia , wakati wa vita vya nchi hiyo 1992 hadi 1995.
 Kesi yake itaendelea baadae mwaka huu kuhusu mashitaka mengine 10 yaliyosalia. Karadzic anatarajiwa kuanza kujitetea tarehe 19 Oktoba.

No comments:

Post a Comment