Friday, June 29, 2012

14 wauawa katika miripuko Baghdad

Watu 14 wameuawa na wengine zaidi ya 45 kujeruhiwa leo katika mashambulizi ya bomu ndani na nje ya mji mkuu wa Iraq, Baghdad. Miripuko hiyo imeufanya mwezi Juni kuwa mwezi mbaya wa umwagaji damu nchini Iraq.
 Mashambulizi hayo yaliongeza idadi ya vifo vya mwezi kufikia 200, ikiwa ni idadi ya juu zaidi tangu mwezi Januari, wakati wanamgambo walipoishambulia nchi hiyo kwa wiki kadhaa baada ya kuondoka kwa jeshi la Marekani.
Mlipuko mkubwa zaidi leo ulitokea katika kitongoji cha Washia wengi cha Washash Magharibi mwa Baghdad. Walioshuhudia wamesema gari moja ya taxi ililipuka nje ya soko moja mjini humo. watu wanane waliuawa na wengine 28 kujeruhiwa kulingana na duru za polisi na madaktari.

 Katika mji wa Taji ulio na wakaazi wengi wa madhehebu ya Sunni Kaskazini mwa Baghdad, magari mawili yaliyokuwa nje ya ofisi ya meya wa eneo hilo yaliripuka na kuwauwa watu watano.
Meya huyo  hakuwemo ofisini humo wakati wa tukio hilo la mapema asubuhi.

No comments:

Post a Comment