Serikali ya Zanzibar imefuta
usajili wa meli tatu ikiwa ni mojawapo ya jitihada ya serikali hiyo
kupunguza matukio vya ajali za baharini.
Miongoni mwa meli hizo zilizoharamishwa ni MV Kalama ambayo pia inamilikiwa na wenye MV Skagit.
Katika ajali hiyo watu zaidi ya 150 walikufa maji.
Hii inakuja siku moja tu baada ya Serikali ya Tanzania kuagiza SUMATRA kufanya kazi yake ipaswavyo.
Katika agizo lake Waziri katika ofisi ya Makamu wa Rais Mohammed Aboud amesema SUMATRA lazima ikague meli zote za Zanzibar kuangalia kama zinastahili kuwa baharini au la.
No comments:
Post a Comment