Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova. |
Watu wanane wanashikiliwa na polisi wakiwemo Madaktari kwa tuhuma za
kuhusika kwenye tukio l a kutupwa kwa mabaki ya miili ya binadamu jana
jioni nje kidogo ya jiji la Dsm
Huku likiendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo,Kamanda wa polisi kanda
maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova ametangaza kuundwa kwa jopo la
upelelezi kuchunguza tukio hilo, ili kubaini taratibu gani zilikiukwa na
kujua aina ya mashtaka itakayowakabili.
Mabaki ya miili iliyotupwa eneo la Bunju Dar es Salaam. |
Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa miili hiyo ilikua katika Taasisi ya
mafunzo ya udaktari IMTU kabla ya kukutwa imetupwa eneo la Bunju.
Taasisi hiyo imekiri kwamba mabaki ya miili ilikua katika taasisi hiyo lakini haijatoa maelezo kuhusu kutupwa kwa miili hiyo.
Kamanda Kova amewatoa wasiwasi watanzania kuwa hakuna mauaji yoyote ya
kimbari yaliyotokea sehemu yeyote nchini hivyo polisi iachiwe ifanye
kazi yake kisha itatoa taarifa hapo baadae.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment