Wednesday, July 23, 2014

Tutajilinda na mashambulizi,Palestina


Palestina imeahidi kuulinda mji wa Gaza dhidi ya mashambulizi ya Israel.
Waziri mkuu wa Palestinian Rami Hamdallah amesema mashambulizi yanayofanywa na Israel yameuharibu vibaya mji wa Gaza.
Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari uliofanyika mjini Ramallah nae Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema mashambulizi hayo yanapaswa kusitishwa kufuatia mauaji ya wapalestina wasio na hatia yanayoendelea.
Zaidi ya Wapelestina 600 wameuawa katika eneo linaloshambuliwa na Israel la Gaza.huku pia huduma za kijamii zikiwa zimeharibika kama vile miundo mbinu ya huduma za maji.

No comments:

Post a Comment