Takriban wakimbizi tisini
waliokuwa wamekwama katikati ya bahari ya Mediterranea kwa siku nne,
hatimaye wameokolewa, kwa mujibu wa shirika la habari la Italia pamoja
na jamaa za wale waliokuwa wamekwama.
Aliongeza kuwa walikuwa wameondoka mji mkuu wa Libya Tripoli, kuelekea pwani ya Italia.
Wahamiaji hao waliokolewa katika mpango wa pamoja kati ya maafisa wa Italia na Libya.
Mapema mwezi huu watu 54 walifariki kutokana na kiu baada ya kuishiwa na maji wakiwa njiani kutoka Libya kuelekea Italia vile vile kwa Boti.
Wahamiaji waliookolewa wamerejeshwa nchini Libya kulingana na taarifa za shirika la habari la Ansa nchini Italia.
Jamaa za wale waliokuwa kwenye boti hiyo walithibitishia BBC kuwa walipatikana.
Wahamiaji wengi kutoka Libya hufariki kila mwaka katika safari zao hatari kuelekea katika kisiwa cha pwani ya Italia cha Lampedusa.
Mmoja wa wahamiaji hao, walisema kuwa walijaribu kuwasiliana na walinzi wa baharini lakini wakapewa nambari nyingine ya simu kupiga ingawa hawakufanikiwa kupata jibu lolote.
Zaidi ya wasomali milioni moja wametoroka nchi yao tangu mwaka 1991, wakati Siad Barre alipompindua rais aliyekuwa mamlakani, na tangu hapo vita havijawahi kuisha nchini Somalia.
No comments:
Post a Comment