Friday, June 29, 2012

Umoja wa Mataifa waonya Sudan dhidi ya ukandamizaji

Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Sudan kukomesha ukandamizaji wakati waandamanaji wakijiandaa kwa maandamano makubwa leo Ijumaa.
 Taarifa ya Navi Pillay imesema matumizi ya mabomu ya kutoa machozi, risasi za moto na aina nyingine za ukandamizaji havitatatua matatizo na kilio cha watu wa Sudan.

 Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema watu kadhaa wamekamatwa tangu maandamano ya kupinga ughali wa maisha kuanza tarehe 16 mwezi huu wa Juni katika mji mkuu Khartoum.
 Maandamano hayo yalianza baada ya rais Omar Hassan al-Bashir kutangaza hatua za kubana matumizi ikiwa ni pamoja na kupandisha kodi na kuongeza bei ya mafuta.
Taarifa ya Pillay inakuja baada ya Sudan kuishambulia kwa maneno Marekani ambayo iliishutumu nchi hiyo namna inavyolishughulikia vuguvugu la maandamano ya umma.

No comments:

Post a Comment