Thursday, November 29, 2012

Umoja wa Mataifa kuwawekea vikwazo viongozi wa M23


Mkuu wa tawi la kisiasa la M23, Jean Marie Runiga.

 


                                                       Licha ya waasi wa M23 kutangaza kujiondoa kwenye mji wa Goma, Umoja wa Mataifa unasema waasi hao hawajaonesha dalili ya kuondoka kabisa na umetoa wito kwa mataifa ye kigeni kutojihusisha na mgogoro kwenye eneo hilo.
Umoja wa Mataifa unatarajiwa kuwawekea vikwazo baadhi ya viongozi wa kundi la waasi wa M23 na vile vile watu wanaowaunga mkono kutoka nje. Kwenye azimio lililopitishwa kwa kauli moja na Baraza la Usalama, Umoja huo umewataka waasi wa M23 kuweka silaha zao chini na kuacha mapigano mara moja na pia kuwaachilia watoto wanaohudumu kwenye kundi lao kama wapiganaji.
Likionesha wasiwasi wake kufuatia taarifa za mauaji, ubakaji na kuajiriwa watoto kwenye kundi la M23, Baraza la Usalama limeelezea nia ya ya kuwawekea vikwazo viongozi wa kundi hilo na watu wanaoaminika kuliunga mkono. Miongoni mwa vikwazo hivyo ni kupiga marufuku ya uuzwaji wa silaha kwa makundi ya waasi wa Kongo.
Serikali ya Kongo ndiyo yenye jukumu la kulinda watu wake
Marais Yoweri Museveni wa Uganda (kushoto), Joseph Kabila wa DRC (katikati) na Paul Kagame wa Rwanda katika mkutano wa viongozi wa Maziwa Makuu juu ya mzozo wa Kivu ya Kaskazini, Novemba 2012.Marais Yoweri Museveni wa Uganda (kushoto), Joseph Kabila wa DRC (katikati) na Paul Kagame wa Rwanda katika mkutano wa viongozi wa Maziwa Makuu juu ya mzozo wa Kivu ya Kaskazini, Novemba 2012.
Vile vile Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Rais Joseph Kabila kuendesha uchunguzi na kuwaadhibu waliohusika na uhalifu huo, kwani "usalama na amani ya Kongo ni jukumu la kwanza la serikali hiyo."
Msimamo huo unafuatia lawama dhidi ya Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo (MONUSCO) ambacho hakikuzuwia kutekwa kwa mji wa Goma na waasi wa M23 wiki mbili iliopita.
Baraza hilo limeyatahadharisha makundi yote ya wapiganaji katika mashambulizi yao dhidi ya walinda amani wa MONUSCO na raia wa kawaida. Baadaye, Baraza la Usalama lilipitisha azimio linaloidhinisha ripoti ya wataalamu kuhusu Kongo.

No comments:

Post a Comment