Wakazi
wa Zanzibar wakiwa wamekusanyika katika Bandari ya Malindi mjini Unguja
Zanzibar jioni ya leo wakati miili ya baadhi ya abiria wa Boti ya
Kampuni ya Seagull "MV Skagit" wakitolewa baada ya boti hiyo kuzama na
kupoteza maisha ya watu zaidi ya 200 hii leo ikitokea jijini Dar es
Salaam.
Askari wa JWTZ wakiwa wamejipanga wakati wa zoezi la kupokea maiti.
Moja ya maiti ikiwa imebebwa na askari
Ni
hali ya huzini Visiwani humo na jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa
ujumla. Ajali hii imetokea ikiwa imepita miezi kadhaa baada ya meli
nyingine ya Abiria kupoteza uhai wa watu visiwani humo.
Meli
ya Mv Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar kuelekea Zanzibar imezama
majira ya saa nane mchana katika maeneo Pungume na Chumbe baada
ya kukumbwa na upepo mkali.
Meli
hiyo inayosadikiwa kuwa na abiria 250 inasemekana imepindukia upande
mmoja na huku abiria wengi wakiweza kuokolewa kutokana na jitihada
mbali mbali kupitia vile vile msaada wa boti za Mv Kilimanjaro, Tug ya
Bandari na vyombo vyengine.
Mpaka
tunandika taarifa hizi ni maiti tatu zilikwishapatikana na kiasi cha
abiria 150 wameokolewa na waliojeruhiwa wanatibiwa katika Hospitali ya
Mnazimmoja.
Taarifa zinaeleza kwamba kulikuwa na watoto takriban 30 na Watalii kutoka nchi mbali mbali wafikao kumi.
Wazamiaji
kutoka Kikosi cha KMKM pamoja na Jeshi tayari wapo eneo la ajali
kusaidia kuokoa maisha ya wananchi waliokumbwa na maafa haya.
No comments:
Post a Comment