Friday, August 24, 2012

Kinyozi aadhibiwa kwa kuwa na uhusiano na mke wa mtu


Polisi nchini Pakistan imesema kinyozi mmoja anapata nafuu katika hospitali moja nchini humo baada ya kukatwa viungo fulani mwilini kufuatia kuwa na mahusiano na mwanamke aliyeolewa katika familia ilio na umaarufu kwenye wilaya ya Okara.

Yousaf Khan, aliye na umri wa miaka 32, alitekwa nyara na wanachama wa familia ya mwanamke huyo na kumdunga macho yake kwa kisu kabla ya kumkata masikio, pua, ulimi na mdomo wake.


Tukio hilo lilitokea siku ya jumanne katika kijiji cha Mirzapur nchini Pakistan. Afisa mmoja wa polisi anayechunguza kisa hicho, Khaliq Riaz, amesema tayari wamewatia nguvuni watu watano.


Hata hivyo, familia ya msichana huyo imesema ilikuwa imetoa onyo kwa Yousaf kuachana na uhusiano huo, lakini hakusikia, na ndio maana wakaamua kuchukua hatua hiyo ili kumuadhibu kinyozi huyo. Uhusiano huo unasemekana ulidumu muda wa miaka miwili.

No comments:

Post a Comment