Wizara ya mambo ya kigeni ya Ethiopia imesema mazishi ya waziri
mkuu Meles Zenawi yatafanyika Septemba 2.
Hii ni kulingana na msemaji wa wizara hiyo, Dina Mufti, aliyezungumza na shirika la habari la AFP.
Mufti hakutoa habari zaidi juu ya mazishi hayo.
Marehemu Meles Zenawi alifariki dunia siku ya Jumaane mjini Brussels alipokuwa anapata matibabu. Zenawi ameiongoza Ethiopia kwa zaidi ya miongo miwili.
Huku hayo yakiarifiwa, mazishi ya kiongozi wa kidini wa kanisa la Orthodox, marehemu Abune Paulos, aliyefariki wiki iliopita akiwa na umri wa miaka 76, yamefanyika leo huko Ethiopia.
Watu zaidi ya 3000, wakiwemo mapadri waliovalia mavazi ya manjano pamoja na watawa na wanasiasa wote walikusanyika pamoja katika kanisa la mtakatifu Selassie mjini Addis Ababa.

No comments:
Post a Comment