Friday, August 24, 2012

Misa ya Wafu yafanyika Afrika Kusini

Waombolezaji nchini Afrika Kusini
Waombolezaji nchini Afrika Kusini

Maelfu ya watu nchini Afrika Kusini wamehudhuria misa ya kuwaombea watu waliouawa katika machimbo ya Marikana ya madini ya Platinum.

Watu thelathini na wanne waliuawa na polisi kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano ya wachimba mgodi huo wakidai malipo zaidi, wiki moja iliyopita.
Misa hiyo ilivurugwa kwa muda kufuatia kuwasili kwa mamia ya wafanyakazi wa mgodi walio katika mgomo, baadhi yao wakiwa wamebeba mapanga.
Misa kama hiyo zinafanyika nchini kote Afrika Kusini.


Rais Jacob Zuma anatarajiwa kuanisha hadidu za rejea kwa tume ya kuchunguza mauaji hayo.
Bwana Zuma hakushangiliwa wakati alipotembelea eneo la tukio la mgodi wa Marikana Jumatano.
Mgogoro huo umesambaa katika migodi mingine ya platinum nchini humo.
Afrika Kusini inazalisha robo tatu ya madini hayo ya Platinum kote duniani na bei ya madini hayo imepanda kutokana na wasiwasi wa kushuka kwa uzalishaji nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment